Elimu ya watu wazima sasa rika zote Kagera

SERIKALI mkoani Kagera kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itaendea kuongeza vitendea kazi na kubuni technolojia wezeshi za kuwafikia wananchi wote ambao hawakubahatika kupata elimu kwa mfumo rasmi ili kutokomeza maadui watatu umasikini, maladhi na ujinga

Akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Muleba katika kilele cha maadhimisho ya juma la wiki ya elimu ya watu wazima kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kaimu Katibu Tawala Bwai Mashauri alisema kuwa kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi mwaka 2022 asilimia 3.3 ya wakazi wa Kagera hawajui kusoma wala kuandika.

Alisema mipango ya Mkoa wa Kagera kupitia idara ya elimu ya watu wazima inaendelea kuweka miundombinu wezeshi na ushawishi mkubwa kwa kila mtu ambaye alikosa elimu kupata elimu na ujuzi hata kama amefikia miaka 60.

Alisema mfumo wa kutoa elimu kwa watu wazima upo kwa njia mbalimbali ikiwemo kuwafundisha Kusoma na Kuandika ,kuwajengea uwezo wa kubuni bidhaa,kujufunza ujasiliamali, kuzalishaji bidhaa na kuwaunganisha katika masoko ili kujenga jamii moja na kuondoka utofauti wa wale ambao hawakusoma kabisa.

Alisema kwa mwaka 2025 watoto ambao huko nyuma hawakusoma kabisa wapatao 402 walijiunga kwenye mfumo Rasmi wa elimu baada ya kufundishwa vizuri na kujua Kusoma Kuandika na kuhesabu.

Alisema mkoa uliwezesha vikundi 3,450 kupata ujuzi wa kutengeneza bidhaa na kufanya ubunifu ili kuongeza kipato cha familia na hizi ni familia ambazo zilijufunza kusoma kuandika pamoja na kufundishwa ujasiliamali.

Kupitia maadhimisho hayo alitoa wito kwa maafisa watendaji waratibu wa elimu kata kushirikiana na watendaji na wenyeviti wa vijiji na mitaa kuweka sheria ndogondogo za kuhakikisha Kila mwananchi anapata elimu kwa mifumo iliyowekwa na serikali bila kujali umri wake ili kuondoa Umasikini mkubwa unaosababishwa na kukosa elimu.

“Natoa wito kwa wanaendesha mifumo ya elimu ya watu wazima kuhakikisha wanaweka vitu vya kuvutia kwani wakikosa elimu ni wengi hivyo wakitaka kujiunga saa nyingine ni ngumu mtu mzima kuja kujifunza kusoma lakini akisikia mnafundisha ujuzi wa kutengeneza bidhaa za kumuingizia kipato atakuja kujifunza na Kwa njia hiyo atajifunza Kusoma ,Kuandika, ujasiliamali na Kwa njia hiyo Mtakuwa mmefukuza maadui watatu kwa wakati mmoja,” alisema Mashauri.

Honoratha Kabundunguru kaimu Afisa Elimu mkoa wa Kagera alisema kuwa moja ya mafanikio makubwa kwa sasa katika elimu ya watu wazima mkoani Kagera ni kuwa na vituo 132 vinavyotoa elimu ya watu wazima kwa rika zote.

Alisema kuwa watoto wa Mtaani waliokusanywa Mtaani kupatiwa elimu ya Kusoma Kuandika na kuhesabu wapatao 4061 kati ya hao 3891 sawa na asilimia 96 wamefahulu na watajiunga na masomo katika mfumo Rasmi wa Elimu huku asilimia nyingine 4 wakiendelea na masoko mpaka watakapofahulu.

Alisema changamoto kubwa kwa sasa ni vituo vya kufundishia kukosa vitendea kazi ,walimu wengi kujitolea kuwafundisha bila malipo,jamii kutotoa ushirikiano wa watoto walipo Mtaani ,walezi kutotimiza wajibu,ajira za utumikishwaji watoto majumbani pamoja na watoto walioacha masomo kwa sababu ya mimba wanaporudi shuleni kutoendelea vizuri na masomo yao.

Idara ya elimu kupitia maadhimisho hayo imeomba mpango wa kutoa elimu ya sekondari kwa njia mbadala kwa wasichana waliokatiza masomo yao kwa sababu ya ujauzito na matatizo mengine ambao ufadhili wake unaisha mwaka 2026 kuangalia namna ya kuongeza na kuuboresha ili kuwasaidia wasichana hao kuunganishwa na mifumo mingine inayotoa ujuzi .

Maadhimisho hayo yalitoa fursa kwa wahitimu wa elimu ya watu wazima kuleta bidhaa zao walizozitengeneza kwa mikono yao kuzinadi kwa wananchi katika siku 4 mfululizo ,kutoa ushuhuda juu ya umuhimu wa kupata elimu , wahitimu kupata vyeti pamoja na kuwaunganisha wahitimu wenye ujuzi katika mifumo ya fedha na masoko ili kukuza uchumi wao.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button