EU yatishia kuiwekea vikwazo Iran

GENEVA : UFARANSA na Ujerumani zimeonya zitarudisha vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran iwapo suluhu la kidiplomasia halitapatikana ifikapo mwishoni mwa mwezi Agosti kutokana na mpango wa nyuklia wa taifa hilo.

Barua iliyotumwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, na Baraza la Usalama, iliyoangaliwa na AFP, imesema mataifa hayo matatu yenye nguvu ya Ulaya yatatumia zana zote za kidiplomasia kuhakikisha Iran haitengenezi silaha za nyuklia, isipokuwa Tehran itaheshimu muda uliowekwa.

Mawaziri wa mambo ya nje wa kundi linalojiita E3 wametishia kutumia utaratibu wa kurejesha vikwazo uliokuwa sehemu ya makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015, yaliyoanza kwa kulegeza vikwazo vya Baraza la Usalama dhidi ya taifa hilo.

Hatua hii inajiri baada ya Israel kuanzisha mashambulizi ya siku 12 dhidi ya Iran mwezi Juni, yaliyoelekezwa kudhoofisha uwezo wa uzalishaji wa nyuklia. SOMA: Iran, E3 waanza mazungumzo mapya

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button