FCC yawavuta wawekezaji IATF

Maonesho hayo yaliyoanza Septemba 4 yanawakutanisha wawekezaji na wafanyabiashara wa Afrika yatafungwa Septemba 10, mwaka huu

ALGIERS, ALGERIA: Tanzania imejipambanua kama nchi salama na yenye ushindani katika kuvutia uwekezaji kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Barani Afrika (Intra African Trade Fair – IATF) yanayoendela jijini Algiers, Algeria.

Maonesho hayo yaliyoanza Septemba 4 yanawakutanisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika kujadili ushirikiano na fursa za biashara.

Katika maonesho hayo, Tume ya Ushindani (FCC) inatoa elimu kuhusu ushindani na ushajishaji wa uchumi kwenye soko nchini Tanzania.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa FCC, Roberta Feruzi, alisema jukumu lao ni kuwaeleza wawekezaji kuwa Tanzania ni soko salama na lenye uwazi na ushindani wa haki.

SOMA: Balozi, bosi Sonatrach wateta fursa za uwekezaji sekta ya mafuta, gesi asilia 

“Tunatoa miongozo kwa wadau wanaotaka kushirikiana na kampuni za ndani katika kununua au kuungana kibiashara na tunarahisisha mchakato mzima,” alisema.

“Kupitia ushiriki wake, Tanzania inalenga kutumia IATF kama jukwaa la kutangaza fursa, kuimarisha urahisi wa uwekezaji na kufungua milango ya ushirikiano wa kibiashara barani Afrika.”

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera, anaongoza ujumbe wa Tanzania. Akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Iman Njalikai, wametembelea Banda la Tanzania na kujadiliana na wawekezaji kuhusu fursa zilizopo nchini.

Taasisi nyingine zinazoshiriki ni pamoja na NEMC, TANTRADE, TMDA. TISEZA, PURA, TFS na ZIPA.

Kupitia maonesho hayo, Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Iman Njalikai alikutana na kufanya mazungumzo na mwenyekiti na mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Algeria (Sonatrach), Rachid Hachichi kwa lengo la kujadili namna gani pande hizo mbili zinaweza kushirikiana katika sekta ndogo ya mafuta na gesi asilia.

Kupitia mkutano huo uliofanyika jijini Algiers Jumapili (Septemba 7, 2025) na kuwaleta pamoja viongozi na maafisa waandamizi kutoka Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) pamoja na wale wa Sonatrach, nchi hizo mbili  pia ziliangazia fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta hiyo muhimu kwa uchumi wa nchi hizo mbili za Afrika.

Mazungumzo hayo yalifanyika Septemba 07, 2025 Jijini Algeris, Algeria na kuhudhuriwa na viongozi wa juu wa Sonatrach na ujumbe wa watanzania uliojumuisha viongozi na maafisa waandamizi kutoka Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA)

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. Google pays $300 on a regular basis. My latest salary check was $8600 for working 10 hours a week on the internet. My younger sibling has been averaging $19k for the last few months, and he constantly works approximately 24 hours. I’m not sure how simple it was once I checked it out.

    This is my main concern………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Earn extra cash every week from the comfort of your home! This flexible part-time opportunity is perfect for anyone looking to make 300-1300 Dollars weekly. Start now and receive your first payment in just a few days. Don’t miss out—join today. Tap on Finance Economy OR Investing..

    Here’s what I do……………….. http://Www.Cashprofit7.site

  3. I just got paid $22k working off my laptop this month!** And if you think that’s cool, my divorced friend has twin toddlers and made over $22620 her first month.details on this website**Want the secret?** Copy this Website and choose HOME TECH OR MEDIA……..

    Here is I started_______ https://Www.CashHive1.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button