Flaviana aibeba Tanzania Jarida la Forbes

DAR ES SALAAM: Mwanamitindo, Flaviana Matata amekua mwanamke pekee kutoka Tanzania kutajwa kwenye Jarida la Forbes Africa ya wanawake hodari wa Afrika waliojitambua na kupata mafanikio kutokana na bidii yao ya kazi kwenye miongo isiyopungua mitatu.

Kwa mara kadhaa jarida hili maarufu limekua likitangaza orodha ya wanawake hodari na wenye maono chini ya miaka 30 na zaidi ya miaka 50 lakini hii ni mara ya kwanza kutangaza orodha ya wanawake hodari na wenye maono ambao umri wao ni kati ya miaka 30 hadi 50.

Katika makala inayomuhusu Flaviana katika jarida hilo la Februari /March 2024, kumeandikwa mengi miongoni mwa yaliyonukuliwa ni

“Wakiwa wanasimulia story yako ukiwa unatokea Afrika wanataka kuzungumzia upande wenye hadithi za umaskini tu ila mimi sina hiyo hadithi ya kuhuzunisha, ni kweli kuna umasikini Tanzania kama ilivyo kwenye mataifa mengine ikiwemo Marekani japo haulingani lakini mimi sijatokea kwenye familia masikini, Baba yangu alinipeleka kwenye shule binafsi nzuri za Kanisa Katoliki”

“Wamagharibi huwa wanapenda kuonesha kwamba wewe ni mtu unayetaka msaada wakati wote lakini nililikataa hilo toka mwanzoni,

Sijatokea kwenye Familia masikini…… hata nilipoanzisha kampuni yangu ya bidhaa za kucha Lavy products walitaka kusema nimeileta bidhaa hiyo kwa ajili ya wanawake wa rangi Fulani kitu ambacho sio kweli, nilianzisha kampuni hii kwa ajili ya mwanamke yeyote anayezipenda kucha zake” amenukuliwa Flaviana Matata.

Habari Zifananazo

Back to top button