Fredy Lowassa akwama Monduli

DODOMA — Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemwacha aliyekuwa Mbunge wa Monduli, Fredrick Edward Lowassa, na badala yake kimemteua Isack Joseph Copriano kugombea kiti cha ubunge wa Jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Lowassa alikuwa mmoja wa wanachama sita waliowania uteuzi huo, wakiwemo Wilson Lengima Kurambe, Sakaya Kabuti Alasheri, Nuru Adam, Bilihuda Hussein Kisaka, na Isack Joseph Copriano ambaye hatimaye alipata uteuzi wa CCM.



