Furaha katika kisiwa cha Uzi-Zanzibar!

WANANCHI wa vijiji vya Kisiwa cha Uzi, Mkoa wa Kusini Unguja wamefurahishwa na hatua ya Serikali ya Awamu ya Nane kujenga daraja na barabara ya kisasa litakalowaunganisha moja kwa moja na Unguja.
Wanasema mradi huu ni mkombozi baada ya miaka mingi ya changamoto za usafiri hasa maji yanapokuwa yamejaa.Daraja la kilomita 2.2 lenye thamani ya zaidi ya dola milioni 14 linatarajiwa kukamilika miezi miwili ijayo, na litafungua milango ya biashara, utalii, huduma za afya na elimu. Pengine litakuwa ni Daraja la pili kwa urefu baada ya Daraja la J.P. Magufuli (kigongo – busisi) lenye urefu wa kilometa 3.2, Tanzania bara
Wananchi wamesema: “Ni ndoto inayoanza kuwa kweli, tunamshukuru Rais Dk. Mwinyi kwa kutimiza ahadi zake. Mwananchi mmoja amesema kwa utani “Nitatembea kwa Kichwa kuonesha furaha yangu.” SOMA: Uwanja wa kisasa wakamilika Zanzibar