Hapi ataka umoja, kuvunja makundi

TANGA: Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Ally Hapi amewataka wanachama wa chama hicho kuvunja makundi ili heshima ya chama iweze kuendelea kuwepo lakini na kupata kura kwa kishindo.
Hayo ameyasema wakati wa kikao kazi cha kampeni za uchaguzi jjjini la Tanga ambapo amewaonya wapambe kuacha kuongeza maneno ya chuki kwa wagombea ambao wamekosa nafasi bali waungane katika kurudisha umoja na mshikamano miongoni
“Naomba mjue kuwa uongozi unatoka kwa Mungu hivyo kukosa nafasi sio sababu ya kuhujumu chama bali huu ni muda wa kuwa wamoja kwa kumuunga mkono aliyekuwepo ili aweze kushinda kwa kupata kura nyingi”amesema Hapi.
Hata hivyo alizitaka Jumuiya za wazazi zote kuwa na mikakati wa kutafuta kura sambamba na kuyafikia makundi yote nje ya chama kura zetu pekee yake hazitoshi, tunahitaji kila mtu atafute kura nje ya CCM.



