Uongozi wa Bayrou watingishwa

PARIS, UFARANSA: WAZIRI Mkuu wa Ufaransa François Bayrou, anatarajiwa kushindwa katika kura ya imani inayofanyika leo Jumatatu. Viongozi wa upinzani wamesema wazi kuwa wataungana kumuondoa kiongozi huyo, hali inayoongeza presha ya kisiasa katika taifa hilo kubwa barani Ulaya.
Kura hiyo muhimu inafanyika mchana na matokeo yake yanatarajiwa kuibua sintofahamu mpya nchini humo, ambayo ni ya pili kwa ukubwa kiuchumi barani Ulaya. Hali hiyo itazidisha mkwamo wa kisiasa ambao tayari umekuwa changamoto kubwa kwa Serikali ya Ufaransa katika kutekeleza sera zake.
Iwapo ataondolewa, hatua hiyo inaweza kuathiri zaidi msimamo wa Ufaransa barani Ulaya, wakati bara hilo likikabiliwa na changamoto nzito ikiwemo vita vya Urusi dhidi ya Ukraine, misuguano ya kibiashara na Marekani, pamoja na nguvu inayoendelea kuongezeka ya China katika uchumi wa dunia. SOMA: Waziri mkuu wa Ufaransa kujiuzulu