Hii ndio pawa ya CCM Namtumbo

SONGEA, Ruvuma: TOFAUTI ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama vingine vinavyowania ridhaa ya wananchi ni namna chama hicho kilivyoweka misingi imara na ya uhalika kuinadi Ilani yake ya 2025-30 huku ikifahamu fika ni namna gani inaenda kupata fedha na kuyatekeleza tofauti na vyama vingine vina maneno matupu.
Hiyo ni sehemu ya kauli ya mgombea urais kupitia CCM, Rais Dk Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wananchi wa Songea Mjin kuomba kura kwa maelfu ya wananchi waliofurika Uwanja wa VETA kumsikiliza Mwenyekiti huyo wa CCM. SOMA: Nchimbi sasa kuwasha moto Njombe

Leo ni siku ya pili ya kampeni za Rais Samia mkoani Ruvuma, ambapo ananguruma Songea Mjini, Namtumbo na Tunduru. Jana, Rais Samia, alimwaga sera zake wilayani Mbinga na Nyasa.



