IAA yapewa jukumu kutangaza elimu EAC, SADC

CHUO cha Uhasibu Arusha(IAA) kimeagizwa kutanua wigo wa elimu katika nchi za Afrika Mashariki(EAC) na Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ( SADC) ili kuitangaza Tanzania katika sekta ya elimu na kuzalisha wahitimu wengi katika sekta mbalimbali pamoja na kupata fursa za ajira na kujiajiri.

Hayo yamesemwa jijini Arusha na Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande wakati wa kutunuku wahitimu 5,854 katika ngazi ya shahada, astashahada na stashahada kwa wahitimu hao.

Amesisitiza IAA kujitanua zaidi katika nchi mbalimbali ili kuwezesha wasomi wengi kuja nchini kusoma ikiwemo kutumia matawi ya chuo hicho kusoma masomo yenye tija yanayotolewa na chuo hicho huku akisisitiza kutumia matokeo ya tafiti wanazofanya na kutumia kama fursa kwa jamii.

Advertisement

“Subiri kichache ili upate kingi ikiwemo kuwa na subra ya mshahara wao mdogo ikiwemo kutafuta fursa za ajira na kuacha choyo kwa wengine katika kutafuta fursa za mafanikio lakini pia tumieni matokeo ya tafiti zetu kama fursa za kujikwamua kiuchumi ikiwemo utatuzi wa ajira na changamoto za wanachi katika eneo husika”

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Chuo, Dk,Mwamini Tulli, ameishukuru serikali na wizara ya fedha kwa kuwezesha chuo hicho kusonga mbele huku akishukuru ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na chuo hicho ambapo kwa mwaka huu 5,854 katika ngazi mbalimbali huku wanaume wakiwa ni 3,601 na wanawake2, 253.