Idadi watumishi zahanati, kituo cha afya waainishwa

DODOMA; SERIKALI imesema idadi ya watumishi wa kada ya afya wanaotakiwa katika ngazi ya zahanati ni kati ya 15-20, wakati kwa kituo cha afya ni kati ya 39-52.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais (Tamisemi), Dk Festo Dugange alipokuwa akijibui swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Anatropia Theonest aliyetaka kujua ni watumishi wangapi wa afya wanatakiwa katika zahanati na kituo cha afya.

“Kwa mujibu wa Muongozo wa Wizara ya Afya wa mwaka (2014 – 2019), umeainisha idadi ya watumishi wa kada ya afya wanaohitajika katika ngazi ya zahanati kuwa ni 15 – 20 na kituo cha afya watumishi kati ya 39 – 52.

“Aidha, idadi hii inaweza kupungua au kuongezeka kulingana na idadi ya wagonjwa wanaopata huduma katika kituo husika.

Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – TAMISEMI inakamilisha kuhuisha mwongozo wa Ikama ya watumishi wa sekta ya afya kwa ngazi ya huduma,” amesema Naibu Waziri.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button