INEC yawataka wasimamizi kufuata sheria.

DAR-ES-SALAAM : WASIMAMIZI na waratibu wa Uchaguzi nchini wametakiwa kufanya kazi kwa weledi na kusoma kwa usahihi katiba, sheria, kanuni na miongozo iliyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwa ajili ya mustakabali wa taifa hadi zoezi la uchaguzi litakapokamilika.

Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Balozi Omar Ramadhan Mapuri wakati wa mafunzo kwa waratibu na wasimamizi wa uchaguzi wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani yanayoendelea kuanzia Julai 21 hadi 23 mwaka huu.

“Tume inawategemea kwa utendaji wenu. Muwajibike ipasavyo katika kipindi chote cha utumishi wenu hadi kukamilika kwa shughuli zote za uchaguzi mkuu,” alisema Balozi Mapuri. SOMA: CUF kushiriki uchaguzi mkuu Oktoba

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpigakura , Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ( INEC), Giveness  Aswile  amesema  mafunzo hayo yalipangwa kufanyika kwa awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza ilifanyika Julai 15–17 mwaka huu.

“Awamu ya pili inaendelea leo katika vituo saba nchini, ikiwemo Dar es Salaam inayoshirikisha mkoa wa Pwani, pamoja na vituo vingine vya Shinyanga, Chake Chake kwa ajili ya mikoa ya Mwanza, Rukwa na Mbeya,” alisema Aswile.

 

 

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button