TAMTHILIA ya Jacob’s Daughters ambayo inachunguza kwa kina maisha ya dada wanne wa mama mbalimbali bali baba mmoja, inatarajia kuzinduliwa kesho.
Tamthilia hiyo inaonesha mabinti walioletwa pamoja na baba yao wakigawanyika kutokana na historia yao na baba yao iliyofichika.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Showmax, tamthilia hiyo ya kusisimua iliyojaa siri za familia, mapenzi haramu na nguvu thabiti ya udugu, inawapa watazamaji nyakati mbalimbali za ugumu wa maisha ndani ya familia.
Katika mfululizo wake watazamaji watachukuliwa katika safari ya hisia iliyojaa mapenzi haramu, ufichuaji wa siri wa kushtua na msuguano mkali wenye lengo la kuokoa familia.
Washiriki wakuu Nuru (Wisher Nakamba), Nana (Angel Mazanda), Caroline (Prisca Lyimo) na Candy (Sia Tarimo), na imeandaliwa na Leah Mwendamseke ‘Lamata’, mwandishi wa hadithi na mkurugenzi.
Katika tamthilia hiyo pamoja na Yakobo (Cojack Chilo), kuwavuta pamoja watoto wake, wadada hao wanakabiliwa na kimbunga hasa mahusiano magumu ya baba yao.
Kadri migogoro inavyozidi katika tamthilia hiyo, udugu wa wadada hao unaingia shakani wakati Jacob alipompenda Diana (Ahlam Khamis Salum).
Uwepo wa Diana unatishia sio tu uhusiano wao wa kifamilia bali pia utulivu wa familia na kuwalazimisha dada hao kusaka njia ya kukabiliana na shida hiyo kwa kurejea katika historia yao na kuamua kupigania mustakabali wa familia.
“Mfululizo huu unatoa maelezo magumu ya mahusiano ya kisasa dhidi ya msingi wa maadili ya kitamaduni,” anasema Lamata.
Jacob’s Daughters ni tamthilia yenye hadithi ya asili ya kusisimua ya kifamilia ya Kitanzania iliyojaa upendo, usaliti na vifungo visivyoweza kuvunjika.