Jaji Masaju asema Ndugai alipenda haki

JAJI Mkuu wa Tanzania, George Masaju amesema Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai alipenda haki.

Jaji Masaju alisema hayo wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa Ndugai kwenye viwanja vya Bunge Dodoma jana.

Alisema wakati alipokuwa Jaji wa mkoa huo alifanya kazi na Ndugai hivyo anamtambua kama mtu aliyependa haki na kwa mchango wake katika ujenzi na ufunguzi wa Mahakama ya Mwanzo Kibaigwa na Wilaya ya Kondoa ili wananchi wapate haki zao.

Jaji Masaju alisema alifanya kazi na Ndugai alipokuwa Katibu Binafsi wa aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Bakari Mwapachu hasa wakati Ndugai alipohitaji kujengwa kwa Mahakama katika Wilaya ya Kongwa.

“Wakati nilipoteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kipindi Ndugai alipokuwa Naibu Spika wa Bunge na alipokuwa Spika alinipatia ushirikiano na mawazo ya kuboresha utekelezaji na upatikanaji wa haki,” alisema.

Jaji Masaju alisema licha ya Ndugai kuwa mchapakazi na kujitoa kwa ajili ya taifa pia alikuwa ana maono makubwa na alipenda maendeleo ya taifa.

Alieleza kuwa wakati wa uzinduzi wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, moja ya mambo aliyoagiza Rais Samia Suluhu Hassan ni watumishi wa serikali kuendelea kutenda haki kwa kuzingatia viapo vyao bila hofu, chuki, upendeleo wala huba na moja ya viapaumbele vya dira hiyo ni haki na Ndugai alipenda kusimama kwenye haki.

Alisema pengo la Ndugai halitazibika kwa sababu pigo lake linaumiza sana, aliwaomba Watanzania na viongozi kuendelea kumuombea.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button