Jambo Group yafariji wagonjwa kituo cha afya Kambarage

MGANGA Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga, Dk Ernest Magula amesema uhitaji wa damu Salama kwenye kituo hicho ni uniti 30 kwa mwezi ili kuweza kutosheleza mahitaji yaliyopo hasa kundi la kina mama wanaojifungua nakutokwa damu nyingi.

Dkt Magula amesema hayo mbele ya Kiongozi Mkuu wa Jambo Media na Kiongozi wa Ubunifu na Chapa ya Jambo Group, Nickson George wakati akikabidhi zawadi ya vinywaji na biskuti kwenye wodi ya wazazi na wagonjwa wa kawaida katika kusherekea chapa mpya ya Selebretika Jamukaya kwenye msimu wa sikukuu ya Krismas na Mwaka mpya.

Dk Magula alipongeza kampuni hiyo kwa kutoa moja ya vifaa katika uchangiaji wa damu kwani hutumia vinywaji kabla ya kumtoa mtu damu pia matumizi yaliyopo ya damu salama kwenye kituo hicho ni uniti 17 haitoshi na mahitaji uniti 30.

“Kila mwezi kina mama 400 wanajifungua na sio wote wenye uhitaji wa damu salama na kitaalamu damu hukaa siku 121 tu na kutotumika tena ila kwenye kituo hiki wanatumia uniti 17 kwa wastani wa mama watatu wanamaliza”amesema Dk Magula.

George amesema wameona kuwakumbuka ndugu na jamaa ikiwa lengo kuu nikutoa zawadi za vinywaji na biskuti vinavyotoka kwenye kampuni hiyo nakutumika hasa pale linapotokea zoezi la uchangiaji damu kulazimika anayetoa kupata kinywaji kwanza.

“Tumetembelea eneo la Kituo cha Afya Kambarage hasa wodi ya wazazi na wagonjwa wa kawaida kuwaona hata wale wanao wasimamamia wagonjwa ambao ni wauguzi na madaktari wanapitia changamoto nakuwafariji kwa kazi hiyo”amesema George.

George amesema tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo zaidi ya miaka 22 wameweza kufarijika kwa mapokeo ya vinywaji wanavyovitengeneza nakuona hakuna budi kuhakikisha msimu huu wa krismasi kusherekea kwa pamoja kwa bidhaa za yumbani yaani Jamukaya.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kituo cha Afya Kambarage, Adolf Nsazukwako amesema zipo changamoto nyingi mojawapo kukosekana uzio hivyo aliiomba kampuni hiyo na wadau wengine wasaidie ili kuhakikisha wazazi wanaendelea kuwa salama zaidi na watoto wao.

Baadhi ya wazazi waliokuwa kwenye wodi Juliana Shija na Fortunata Athanas wamesema kituo kimewapa huduma nzuri nakuishukuru kampuni ya Jambo group kwa msaada walioutoa.

MWISHO.

Habari Zifananazo

Back to top button