Jamii yahimizwa mazoezi kuepuka magonjwa

JAMII imehimizwa kujiunga na vyama mbalimbali vya mazoezi ili kuepukana na majongwa yasiyoambukizwa ikiwemo kisukari, saratani na mengineyo.

Mkurugenzi Msaidizi Magonjwa yasiyoambukizwa kutoka Wizara ya Afya, Dk Omary Ubuguyu amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa matembezi yaliyoandaliwa na TANCDA.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari Dk Omary amesema kuwa matembezi yamehudhuriwa na zaidi ya watu 1000 kutoka vyama mbalimbali.

“Tunaishukuru Serikali kwa kufunga barabara ya Coco beach kwa lingo la kuhimiza wananchi kufanya mazoezi. Hili ni jambo la pongezi kwao na tunaahidi kuunga mkono,”alisema

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Kisukari Tanzania TDA Profesa Andrew Swai ameshauri wananchi kupunguza matumizi ya sukari na chumvi kwa wingi wa lengo la kujikinga na magonjwa.

“Ukitumia asali tayari imejaa sukari kwa kuwa ni majimaji huna njia ya kuzuia ikae nje, itaingia mwilini haraharaka na itakuletea matatizo, ndio sababu tunawaambia watu wasitumie sukari au asali ikizidi inachoma ndani na kusababisha magonjwa mbalimbali “amesema

Habari Zifananazo

Back to top button