Deprecated: htmlspecialchars(): Passing null to parameter #1 ($string) of type string is deprecated in /home/habarileoacc/public_html/wp-includes/formatting.php on line 4732

Vitendo vya ukatili mashuleni vidhibitiwe

Deprecated: htmlspecialchars(): Passing null to parameter #1 ($string) of type string is deprecated in /home/habarileoacc/public_html/wp-includes/formatting.php on line 4732

DAR-ES-SALAAM ; WADAU wa elimu wamesema malezi ya watoto yanapaswa kushirikisha wadau  wengi ili kuhakikisha ulinzi wa watoto  wakiwa mashuleni unaimarika kwa lengo la kulinda ustawi wa maendeleo ya mtoto.

Akizungumza na wazazi katika Mahafali ya 15 ya Shule ya Msingi ya Moga iliyoko jijini Dar-es-salaam.Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Moga, Pastor Leonard  Ntimba amesema vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia  kwa watoto mashuleni vinazidi kuongezeka na kuhusisha baadhi ya walimu kufanya matukio mbalimbali ya kuwadhalilisha  watoto wakiwa mashuleni.

“ ni aibu kusikia ama kuona mwalimu anamdhalilisha mtoto ni aibu sana na haiajwahi kutokea miaka ya nyuma  mwalimu siku zote ndio tegemeo la ulinzi wa mtoto akiwa shuleni  tunapaswa kubadilisha tabia na kufuata miongozo ya uangalizi wa watoto’, alisema Pastor Leonard,

Aliongezea “ tunajua wazazi pia mnamajukumu mengi  lakini malezi ya mtoto  yanahitaji  uangalizi wa pande zote mbili mwalimu, mzazi na jamii kwa ujumla hasa mtoto akiwa shuleni hili ni jukumu la kwetu sote,; alimalizia.

SOMA : Serikali yaja na mikakati ya kukomesha ukatili wa watoto

Pia ameziomba mamlaka za sheria kufuatilia na kusimamia vyema sheria za ulinzi wa mtoto ili kuhakikisha ustawi wa maendeleo ya mtoto unalindwa ndani ya jamii.

Deprecated: htmlspecialchars(): Passing null to parameter #1 ($string) of type string is deprecated in /home/habarileoacc/public_html/wp-includes/formatting.php on line 4732

Deprecated: htmlspecialchars(): Passing null to parameter #1 ($string) of type string is deprecated in /home/habarileoacc/public_html/wp-includes/formatting.php on line 4732

Habari Zifananazo

Back to top button