Jeshi la polisi Tanga lakabidhiwa magari

TANGA: Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dk Batilda Buriani amekabidhi magari tisa kwa jeshi la polisi mkoani hapa ambayo yatasaidia kuongeza ufanisi kwenye utekelezaji wa majukumu yao.

Katika magari hayo, moja la Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi na magari manane ni kwa ajili ya maofisa upelelezi wa jeshi hilo waliopo kwenye wilaya nane za mkoa huo.

Akizungumza mara baada ya zoezi la kukabidhi magari hayo, RC Batilda alisema magari hayo yametolewa na serikali ili kutatua changamoto ya vitendea kazi ambavyo vilikuwa vinalikabili jeshi hilo.

“Vyombo vyote vya usalama vimeweza kukabidhiwa vyombo vya usafiri na Rais Samia ili kuendelea kuhakikisha amani na utulivu wa nchi unaimarika,”alisema RC Batlida.

Alisema kuwa katika mkoa huo vyombo vyote vya usalama viliweza kukabidhiwa usafiri ikiwemo jeshi la Zimamoto ili kuendelea kufanyakazi zao bila ya usumbufu wowote ule.

Naye, Almachius Mchunguzi aliishukuru serikali ya awamu ya sita kwa muendelezo wa kutoa usafiri ikiwemo ni muendelezo tangu ameingia madarakani.

Alisema kuwa katika kipindi cha uongozi wake jeshi hilo limeweza kupitia maboresho makubwa kutokana na serikali kuendelea kuimarisha utendajikazi wao kwa kuwapatia vitendeakazi lakini na maboresho ya stahiki zao mbalimbali.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button