We will continue with our topic Kazini
Sikiliza ana shamba kubwa,Anafanya kazi shambani pamoja na watoto wake ,Kila mwaka wanapanda mbegu nzuri za mahindi,mpunga ,maharage,na mihogo.Sikiliza hapendi mtoto mvivu,siku moja ,Mashaka alichelewa kufika shambani ,Mama yake alimwambia ,””Ukichelewa tena utalima peke Yako wakati sisi tumekwenda nyumbani,”Toka siku ile ,Mashaka hajachelewa tena kazini.Watoto wa Sikiliza wanajua lazima Kila mtu afanye kazi.
Sikiliza Anafanya kazi kwa bidii ,na watoto wake pia wanafanya kazi kwa bidii ,Mwaka Jana Sikiliza na watoto wake walipata mavuno mazuri sana, Sikiliza Hana shida ya chakula ,watoto wake Kila siku wanakula chakula bora,Mara kwa mara Tatu huenda sokoni kununua samaki ,vitunguu na nyama ,Kila siku anawapa watoto wake chakula Cha kuchukua shuleni .jioni walirudi,wanamsaidia Kazi shambani ,Mashaka ni hodari sana shuleni, Walimu wake wanampenda sana .Chausiku ameanza kusoma juzi tu,Sijali bado mdogo.
Maneno muhimu
Kuanza kazi, to begin working,to start
Kufanya uzembe kazini,. to be careless at work
Kuwahi kazini;kuchelewa,. to be on time for work;to be late
Kupoteza;kupoteza muda, to lose;to waste time.
End of our topic