Jitokezeni kupiga kura – Bananga

DAR ES SALAAM: KATIBU wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Bananga amewataka wananchi kujitokeza kupiga kura Oktoba 29 katika Uchaguzi Mkuu na kusisitiza kuwa hakuna mtu yeyote atakayevuruga uchaguzi au kufanya maandamano.

Bananga alitoa wito huo wakati akifunga mkutano wa kampeni za CCM Kata ya Kigamboni, mkoani Dar es Salaam

Ameitaka jamii kutokuwa na wasiwasi kwasababu wataenda kupiga kura kwa amani na kurudi makwao kwa amani na kuendelea kisubiri matokeo kwa utulivu.

“Kwanza niwahakikishieni hakutakuwa na maandamano, kwani maandamano hayawezi kuratibiwa Marekani halafu yafanyike nchini Tanzania, hakuna mtu atakayejitokeza kufanya maandamano,” amesema.

Pia, Bananga amemtaka mgombea udiwani wa Kata ya Kigamboni, Dotto Msawa, kushirikiana na wenyeviti wa serikali za mitaa kuhakikisha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu wanapatiwa mikopo ya asilimia 10 kutoka halmashauri.

Amesema mikopo hiyo ni kwa ajili ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ambao hawana dhamana za kukopesheka kwenye mabenki.

“Hakikisha wanaopata mikopo ni wanawake wa kawaida ambao hawana dhamana za kusaidia kupata mikopo, wapeni hawa wakajikwamue na familia zao kwa kufanya biashara ndogo ndogo,” amesema Bananga

Naye diwani wa kata hiyo, Dotto Msawa aliwaomba wananchi wa Kata ya Kigamboni na Watanzania kwa ujumla kumpigia kura nyingi Samia Suluhu Hassan, kwa sababu amefanya mambo mengi mazuri ndani ya kipindi cha miaka minne ya uongozi wake.

“Mama Samia alipoingia madarakani ndiye aliyesababisha kujengwa Shule ya Sekondari Paul Makonda tena ya ghorofa yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 1.5, ametoa fedha kwa ajili ya elimu bure kwa watoto wetu, meza na madawati kwa shule za sekondari. Tulikuwa na zahanati ndogo lakini sasa amejenga kituo cha afya,” amesema.

Pia, Msawa amesema katika uongozi wa Samia wamewapatia gari la kubeba wagonjwa, mashine ya X-ray na ametoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya barabara zote za kata hiyo.

Aidha, Msawa amemuhakikishia Bananga kuwa endapo atachaguliwa ataendelea kusimamia vizuri fedha za mikopo kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kama alivyofanya kipindi kilichopita.

“Mwenezi, kuhusu mikopo ya asilimia 10 ya vijana, wanawake na wenye ulemavu niliisimamia vizuri, kuanzia kwa vijana wa bodaboda, mamalishe na wengine wote. Katika kata yangu niliyoiongoza hatukuwa na tatizo kwa makundi hayo kupata mikopo, tuko vizuri,” amesema.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..

    .

    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button