Jubilant Andrew: Mitindo ipewe thamani inayostahili

DAR ES SALAAM: MDAU mkubwa wa mitindo nchini, Jubilant Andrew ameshauri kuwa Serikali, wadau na wawekezaji wanapaswa kuweka nguvu sekta ya mitindo, na kuipa thamani sawa ilivyo kwa sekta ya muziki, maigizo.

Akizungumza leo September 6, 2025 Dar es Salaam, Jubilant amesema hatua hiyo itaifanya sekta ya mitindo kukuwa na kuwapa thamani wanamitindo wa Kitanzania.

Akizungumzia upande wa nguvu ya serikali, ameshauri kuwa kuna haja ya kuanzisha mafunzo rasmi, pamoja na kufungua akademii za vijana kujifunza mitindo kama ilivyo kwa nchi zilizoendelea.

“Pia uwepo ushirikiano wa kimataifa kurahisisha visa, ruhusa na network, ili models wa Tanzania wafanye kazi nje connection kwa ujumla za kimataifa,” amesema Jubilant.

Ameendelea kuiomba serikali, kuitangaza nchi kwa kutumia wanamitindo kama mabalozi wa utalii na utamaduni wa taifa.

“Ajira na masoko kusaidia ‘models’ kupata nafasi kwenye fashion shows, matangazo ya biashara, na kampeni za kimataifa,” amesema Jubilant Andrew.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button