Jubilee Health Insurance wajizatiti kuboresha huduma

DAR ES SALAAM; KAMPUNI ya Jubilee Health Insurance imesema inaendelea kutekeleza mikakati madhubuti inayolenga kuimarisha huduma za bima ya afya Tanzania, kwa kuzingatia uzoefu wake katika sekta hiyo hapa nchini.

Hayo yamebainishwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Dk Harold Adamson, katika taarifa iliyotolewa kwa waandishi habari na kueleza kuwa kampuni hiyo ina jukumu muhimu katika kubadilisha jinsi bima ya afya inavyowahudumia watu binafsi, familia na biashara.

Dk Harold Adamson

Amesema kuwa kampuni itakuwa mstari wa mbele kuweka kipaumbele kwa huduma za afya zinazopatikana kirahisi kwani katika miaka iliyopita kampuni hiyo chini ya uongozi wake imeweza kufanya kazi kuhakikisha kwamba Bima ya Afya ya Jubilee inabaki kuwa mshirika wa kuaminika katika afya na ustawi kwa wateja wote nchini Tanzania.

“Katika Bima ya Afya ya Jubilee, tunalenga kutoa suluhu za bima ambazo sio tu zinafanya kazi bali pia zina mchango mkubwa katika kulinda ustawi wa wateja wetu,”  amesema Dk Adamson.

Amesema chini ya uongozi wake, kampuni hiyo imeanzisha sera na mipango inayobadilisha hali ambayo inakabili changamoto mpya za afya huku ikihakikisha wateja wanapata huduma bora.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button