Jukwaa la ubunifu kuanza Sept 28

JUKWAA la Ubunifu nchini (Tanzania Fashion Festival) Msimu wa 7 unatarajia kufanyika Septemba 28, 2024 katika ukumbi wa Terrace Slipway uliopo Masaki jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Spotileo muandaaji wa jukwaa hilo, Deogratius Kithama ‘Mzee wa Fashion’ amesema kila msimu kunakua na utofauti kwani msimu huu mgeni rasmi anatarajia kuwa Miss Tanzania Tracy Nabukeera.

Amesema wamechukua warembo wengi kutokana na muitikio mkubwa zaidi na kupelekea kuwapa nafasi zaidi.

“Lengo la jukwaa hili ni kuendeleza na kukuza Sanaa za maonyesho kuibua na kuunga mkono vipaji vipya vinavyochipukia kupata nafasi ya kuonyesha Mavazi yao bure bila gharama yoyote Ile unachotakiwa ni kuandaa Mavazi yako na kuja kuonyesha katika jukwaa la Tanzania Fashion Festival.hil.”amesema Deo.

“Tamasha hilo linalotarajia kuwakutanisha mastaa mbalimbali ikiwemo wasanii wa muziki Bongo Fleva, filamu, viongozi na sanaa za maonyesho nchini limezinduliwa rasmi na linatarajiwa kufika tamati tarehe 28.”

“Kwa kutambua mchango wangu katika tasnia ya ubunifu wa mavazi nchini hivyo niliamua kuandaa jukwaa hili kuibua wabunifu wachanga na kuzidi kuipa nafasi tasnia ya mavazi nchini,”amesema Deo.

Hata hivyo amesema jukwaa hilo linafungua fursa mbalimbali kwa wanamitindo wenyewe hadi wabunifu nje na ndani ya nchi kujulikana kutokana na wageni wanaohudhuria kupenda bunifu zinazopita jukwaani.

Aidha, ameeleza kuwa mwaka huu litakuwa wa tofauti na misimu iliyopita kuandaa kwa kuwa Ili kunogesha jukwaa hilo lenye kufungua fursa za kibiashara na kuwaomba wadhamini wajitokeze kwa wingi.

Habari Zifananazo

Back to top button