JWTZ yaonya wanaotumia jeshi kupotosha mitandaoni

JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesisitiza kuwa litaendelea kushirikiana na vyombo vingine vya Usalama na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuwabaini na kuwachukulia hatua za kisheria wote wanaojihusisha na kulitumia jeshi kutoa taarifa za upotoshaji.

Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ Kanali Bernard Mlunga ametoa onyo hilo wakati wa kutoa taarifa kwa umma.

Amesema :”Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linautaarifu umma wa Watanzania kuwa tangazo linaloonekana likisambaa mtandaoni lenye maudhui ya maandamano ni uzushi wenye lengo la kuwahadaa wananchi na kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani nchini, hivyo lipuuzwe.”

“Aidha, JWTZ linakemea tabia inayokithiri ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijami inayolihusisha Jeshi na siasa kwa lengo la kupotosha umma na kuzua taharuki.”

Amesema JWTZ litaendelea kushirikiana na Vyombo vingine vya Usalama na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania litawachukulia hatua za kisheria watakaobainika kufanya hivyo.

“JWTZ litaendelea kushirikiana na Vyombo vingine vya Usalama na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuwabaini na kuwachukulia hatua za kisheria wote wanaojihusisha na upotoshaji huo.”

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button