Kadinali Pengo alikuwa zaidi ya kiongozi wa Kanisa

DAR ES SALAAM; Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo aliyefariki dunia jana Februari 19, 2026, alikuwa zaidi ya kiongozi wa Kanisa; alikuwa sauti ya dhamiri, mwalimu wa maadili na alama ya utulivu katika nyakati za mabadiliko ya Taifa na Kanisa.
Safari yake ya maisha, iliyoanzia kusini-magharibi mwa Tanzania hadi ngazi za juu za uongozi wa Kanisa Katoliki duniani, ni simulizi ya huduma, uaminifu na kujitoa bila kujihifadhi.
Kadinali Pengo alizaliwa Agosti 5, 1944, mjini Sumbawanga, mkoani Rukwa. Alikulia katika mazingira ya unyenyekevu, safari ambayo ilimjenga kuwa kiongozi wa watu wote maskini na wenye uwezo, waumini na wasiokuwa waumini.
Aliingia katika huduma ya kipadre akiwa na ari ya kutumikia, na kwa miongo kadhaa alitumia maisha yake kuimarisha imani, maadili na mshikamano wa jamii.

Mwaka 1992, aliteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam. Kwa miaka 27 mfululizo, aliiongoza dayosisi hiyo muhimu zaidi nchini, katika kipindi kilichoshuhudia mabadiliko makubwa ya kijamii, kisiasa na kiimani.
Uongozi wake ulijengwa juu ya busara, nidhamu ya mazungumzo na msimamo wa haki—akisisitiza amani, maridhiano na utu wa binadamu.
Mwaka 1998, Kadinali Pengo aliandika historia alipoteuliwa na Papa kuwa Kadinali, akawa Kadinali wa pili wa Tanzania, akitanguliwa na Laurian Rugambwa.




I started this as a simple side hustle, and last month I made a little over $6,137 just working a few hours a day from my phone. If you want to check out how it works, the website has all the details.
Here—>> http://www.giftpay7.vip