Kagame Tshisekedi watakiwa kufanya mazungumzo

GOMA : RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, amekutana na Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kujadili kuongezeka kwa ghasia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo wanajeshi 13 wa Afrika Kusini wameuawa.

 Rais Ramaphosa na Kagame wamekubaliana juu ya umuhimu wa kumaliza mapigano na kurejesha mchakato wa mazungumzo ya amani kwa kuhusisha pande zote zinazohusika.

 Haya yanajiri wakati Rais wa Kenya, William Ruto, alipotangaza kuwa Kagame na Rais wa Congo, Felix Tshisekedi, watashiriki katika mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kesho. Vilevile, Umoja wa Afrika unatarajiwa kukutana leo ili kujadili mzozo huo.

 Taarifa za hivi punde zinaeleza kuwa waasi wa M23 wamechukua udhibiti wa uwanja wa ndege wa Goma.

SOMA: Tahadhari ya usalama yatangazwa Congo

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button