Kagera iko salama Oktoba 29 -Mwasa

KAGERA: Mkuu wa Mkoa Kagera, Hajath Fatma Mwasa amewahakikishia wananchi wa mkoa huo kuwa hakutakuwa na vurugu yoyote siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 mwaka huu kama ambavyo hofu inasambazwa mitandaoni.

Akizugumza na makundi mbalimbali ya wananchi wakiwemo maofisa usafirishaji (bodaboda), wafanyabiashara na wanachi kwa ujumla, RC Mwasa alisema kuwa ulinzi umeimarishwa huku akiwataka wananchi kujitokeza kupiga kura.

Alisema wengi wanaohamasisha vurugu wako nje ya nchi hivyo wananchi wanapaswa kuwakataa na kukataa uzushi huo wa vurugu na kudai kuwa moja ya haki ya wananchi kikatiba ni kuchagua viongozi wanaowataka ambapo.

Alisema maneno ya uzushi yanayoendelea yamekuwa yakimtaja yeye moja kwa moja kwa shutuma ambazo siyo za kweli kuwa anahusika na mgombea aliyehama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kwenda kugombea ACT Wazalendo zinapaswa kupuuzwa moja kwa moja kwani yeye kwa nafasi yake anahusika na kuchangia maendeleo ya mkoa na sio kushiriki kugombea.

“Wako watu hata mimi wananizushia maneno, wengine nikasikia juzi wananipa onyo, nikamsikiliza yule mtu nikasema nakusamehe tu, siwezi kuua sisimizi kwa nyundo, mimi nina watoto wangu wengi maofisa usafirishaji ambao wananilinda wakati wote, atakayenivaa watamvaa,” alisema Mwassa.

“Nimezaliwa CCM nitafia CCM msilitumie jina langu vibaya kama kuna mtu alikuwa rafiki yangu akahamia upinzani siwezi kushiriki nawahakikishia hata angekuwa mtoto wangu wa kumutoa tumboni nimemzaa akihama chama akaenda kugombea chama kingine siwezi kujihusisha naomba jina langu lisitumike vibaya,”alisema Mwassa.

RC Mwassa amesema kwa nafasi yake hawezi kufanya kampeni au kuhudhuria mkutano wowote wa kampeni na haoni sababu ya kufanya hivyo kwa sababu siyo jukumu lake bali la viongozi wa chama.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button