Kairuki aahidi kujenga barabara tisa miaka mitano

DAR ES SALAAM: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kibamba kupitia Chama Cha Mapinduzi, (CCM) Angellah Kairuki amesema endapo atapewa ridhaa ya kuongoza jimbo hilo atahakikisha barabara tisa zilizilizopo katika kata ya Goba zinajengwa ndani ya miaka mitano.
Akizungumza wakati wa Kampeni zake katika kata ya Goba jijini Dar es Salaam Kairuki amesema barabara atakazojenga ni
barabara za Goba Mjengo, Mtipesa, kwa Makonda,Kwa mwaipopo, TAG Matosa ,kwa Awadhi, Maendeleo sheraton,Country bus na Tatendo.
Vipumbele vingine aliyoanisha ni
kumaliza changamoto zilizobaki za ujenzi wa kituo cha polisi kwa kujenga uzio na kununua gari la polisi ili kituo hicho kifanye kazi kwa ufasaha.
“Ninajua changamoto ya mgogoro wa DDC wapo wananchi wamesumbuka kupata hati miliki nitapoingia madarakani nitafanyia kazi kupata suluhu,hitaji la daraja katika shule ya sekondari Goba mpakani na madarasa ya kidato ya tano na sita nitalitekeleza.
Ameongeza “Kwa mtaa wa Muungano natambua hitaji ya shule ya msingi nitalifanyia kazi watoto wasivuke mto natambua hitaji ya kivuko cha lami litakalounganisha mtaa wa Muungano pamoja na Mivumoni na kwa elimu mtaa wa Muungano unahitaji shule ya msingi na sekondari imekamilika kwa asilimia 90 nitawahakikisha itaanza kutoa huduma.
Kairuki amesema kuwa kwa upande wa mtaa wa Kunguru atahakikisha anajenga barabara za ndani na kushughulikia changamoto ya mtoto aliyetelekezwa na baba yake apate huduma.
Amesena kwa upande wa mtaa wa Kisuku atatekeleza hitaji ya soko ,barabara za ndani,kalvat na barabara ya Zuruni huku akiwahakikishia ujenzi utakuwa kipaumbele.
“Natambua umuhimu wa daraja la kwa baba Deni na vingine niwahakikishe tutajenga daraja la kwa Silayo.
Amesema kwa Shule za Goba kuna changamoto ya uzio,maeneno na ukarabati watatengeneza mazingira bora na kwa zanahati ya goba watapambana ipandishwe hadhi kuwa kituo cha afya na kufanya kazi saa 24.
“Kuna changamoto ya maeneno ya kuzikia tutalifatilia kwa kushirikiana na mitaa na halmashauri kupata maeneo.
Kairuki amebainisha kuwa kwa matosa atatatua hitaji la barabara inayounganisha Njia nne matosa kwenye Temboni atahakikisha lijengwe pia changamoto ya barabara,vivuko na shule Kulagwa itaisha.
“Endapo mtamchabgua Samia Hassan,endapo mtanichagua mimi na diwani tutakamisha hospitali zetu na kuboresha huduma na kuongeza vifaa tiba,
Kwa elimu tutakarabati shule ziwe za kisasa tutaongeza madawati nitapamba shule ya mahitaji maalumu inapatikana nitaweka pia katika shule zetu.
Amesema kwa Maji licha ya kuwepo kwa kiasi kikubwa atahakikisha hakuna bili za kubambikizwa kwa kuwashawishi mita za luku za maji kuanza.
“Serikali kupitua halmashauri inatoa mikopo tutajihadi vikundi vingi vinapata mkopo,tutaleta mafunzo ya biashara,tutaweka fursa za ajira kwa bodaboda tunajua shida zenu tutatoa mikopo kuweza kununua bodaboda na akinamama watapata mikopo ,”amesisitiza
Kairuki ameeleza kuwa atasimamia urasimishaji wa ardhi kuwe na mfumo ulioboreshwa,kwa masoko atahakikisha yanajengwa,upatikanaji wa usafiri wa daladala utqkuwepo,wenye ulemavu wananufaika na fursa na vijana watanufaika na mazingira mazuri ya biashara.




I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com