Kairuki ataka Kibamba wafanye kweli Oktoba 29

DAR ES SALAAM:MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Kibamba kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Angellah Kairuki, amesema kwa kazi kubwa iliyofanywa na mgombea urais wa chama hicho Dk  Samia Suluhu Hassan katika jimbo hilo  anastahili pongezi ya kupigiwa kura za kishindo Oktoba 29, mwaka huu.

Akizungumza wakati wa kampeni zake jijini Dar es Salaam katika kata ya Kwembe Kairuki, amesema wananchi wanapaswa kupiga kura za ndio ili kupata mafanikio zaidi.

“Walisema chanda chema huvishwa  pete tukakivishe pete Chama Cha Mapinduzi, tukamvishe pete mama yetu Dk  Samia Suluhu Hassan kwa kumpatia kura nyingi za kishindo, ili na mimi nikiwa nyuma yake kumsaidia  kuwa mbunge kwa jimbo la kibamba lakini msimsahau Mgombe diwani wa Kwembe,Haji Konde,” amesema.

Amesema serikali imefanya mambo makubwa ambayo ni pamoja na kuweka maktaba katika Shule  ya Msingi Kwembe iliyogharimu shilingi milioni 10, ujenzi madarasa uliogharimu sh milioni 40 katika Shule ya Msingi Kwembe na kusaidia  wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu .

Amesema  serikali  ya CCM imewekeza zaidi ya sh bilioni 6. 6 kwa elimu ya sekondar,i lakini sambamba na hilo imewekeza sh bilioni 5. 8 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Dar es Salaam Girls ambayo iko katika kata hiyo.

“Shule  ya sekondari ya King’azi   walimu wamejengewa nyumba, tuliweza  kununua samani  katika shule ya Dar es salaam kwa takriban shilingi milioni 100. 8 ili kuhakikisha inakuwa na mandhari nzuri na watoto wetu hawa wasikae chini,” amesema.

Kwa upande wa barabara amesema waliwekeza katika matengenezo ya barabara ya St Joseph Millenia na Kwembe

Eneo la afya waliwekeza katika kuboresha zahanati  ya Amani kwa gharama zisizo pungua sh milioni 580 na kununua   dawa na vifaa tiba  uhakika wa upatikanaji wa dawa kwa zaidi ya 98%.

Kwa upande wa uwezeshaji wananchi kiuchumi, ameeleza kuwa wametumia Sh milioni 32. 1 kwa ajili ya kukopesha kwa makundi maalum yenye uhitaji makundi 26, wakiwemo wanawake ,vijana pamoja na watu wenye ulemavu.

“Upande wa maji  mtandao wa usambazaji wa maji umejengwa kupitia mradi wa usambazaji wa maji kwa Dar es salaam linaendelea pia katika kata yetu ya Kwembe, lakini sambamba na hilo tunao mradi kwa Kingazi B kwa ajili ya kuongeza msukumo wa maji na suala hili limefanyika vizuri na kupitia ujenzi wa tenki yetu ya Bangulo na sasa unaendelea na majaribio tunaamini utaongeza sana upatikanaji wa maji kiwango cha juu  cha upatikanaji wa maji Kwembe ni asilimia 95,” amesema mgombea huyo.

Amesema upande wa  wa King’azi wameendelea kuboresha mradi wa maji  kwa kutumia shilingi milioni 33. 3 na tayari wateja wamenufaika 3, 154 na kazi inaendelea.

“Lakini tunaendelea pia kuwekeza katika miradi midogo ya upanuzi wa maji tumetekeleza Malamba mradi wa  sh milioni 157, mradi wa Kwembe Babu  Sh milioni 66. 9 na wanufaika 1995 tayari wanapata maji,” amesema.

 

Habari Zifananazo

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button