Kalamu ya Mwandishi: Nyenzo muhimu ya amani uchaguzi mkuu

VYOMBO vya habari ni wadau muhimu katika uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu. Kupitia vyombo vya habari wananchi wanatarajia kupata taarifa sahihi kuhusu yanayoendelea kabla, wakati na hata baada ya uchaguzi, hivyo umakini, uwazi, na kutoa habari zenye usahihi zisizo na uchochezi ndicho kitakachofanya uchaguzi huo kuwa wenye utulivu na usalama.
Kuimarika kwa amani, usalama na utulivu wa nchi katika kipindi hicho inategemea kalamu za waandishi wa habari zitatumika vipi kwani zikitumika vizuri zitasaidia kuepusha machafuko na zikitumika vibaya zinaweza kuwa chanzo cha machafuko na kuweka maisha ya Watanzania wengi katika hali ya hatari.
Katika kuhakikisha waandishi wa habari wanajua nini wanatakiwa kufanya ili kufanya kazi yao kwa ufanisi katika kipindi cha uchaguzi wadau wa sekta ya habari na utangazaji Kanda ya Mashariki wamewataka waandishi wa habari kuwa makini na maudhui wanayopeleka kwa wananchi.
Ushauri huo umetolewa wakati wa mafunzo maalumu kwa waandishi wa habari kuelekea uchaguzi mkuu yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Jeshi la Polisi Tanzania na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kupitia Idara ya Habari Maelezo na Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB).
Akifungua mafunzo hayo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi amewaagiza waandishi wa habari waandike habari za uchaguzi mkuu kwa kuzingatia uzalendo badala ya masilahi binafsi. Profesa Kabudi anawasisitiza waandishi wa habari waandike habari za uchaguzi zenye maslahi ya taifa na wajiepushe na vitendo vya rushwa sambamba na kutumia vyombo vyao kujenga tija kwa umma.
Pia, aliwataka watumie kalamu zao kueleza sera za vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi kwa usawa na si kuandika habari za uchochezi. “Watanzania watangulize uzalendo mbele, hatuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania, tuhakikishe uchaguzi unakuwa wa amani na wanahabari zingatieni misingi ya taaluma, kuweni wazalendo, uchaguzi uwe wa amani,” anasema. Meneja wa Habari wa TCRA, Andrew Kisaka anawataka waandishi wa habari kuepuka kuripoti taarifa za uchochezi zinazoweza kuchochea migogoro na vurugu wakati wa uchaguzi mkuu.
Kisaka anasema ili kuepuka taarifa za uchochezi vyombo vya habari vinapaswa kujua na kuzingatia wajibu wao wakati wa uchaguzi ambao ni kutopendelea wakati wa kutoa taarifa, kuhakikisha uwazi kwenye mchakato wa kisiasa, kutoa jukwaa kwa wagombea na wapigakura kujadili mada muhimu kwa usawa. Anasema ili kuepuka kufanya uchochezi waandishi wa habari wanapaswa kuzingatia na kujua viashiria vya migogoro vikiwemo vitisho, manyanyaso, na vurugu dhidi ya baadhi ya makundi.
Anataja viashiria vingine kuwa ni maneno ya chuki kuwalenga wagombea, wapigakura au vyama vya siasa kwa vitisho na hofu na kushambulia mchakato wa upigaji kura, vituo vya kupigia kura ama viongozi wanaotoa uamuzi. Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime anawataka wanahabari kutambua na kuheshimu mipaka ya kila mmoja katika utekelezaji wa wajibu na majukumu yao wakati wa uchaguzi huo.
Akifanya wasilisho wakati wa mafunzo hayo kuhusu wajibu wa waandishi wa habari na Jeshi la Polisi katika uchaguzi mkuu, Misime anasema uchaguzi ni kipindi muhimu katika nchi yoyote ile na wananchi wanashiriki ili kutimiza haki yao ya msingi ya kuchaguliwa au kuchagua viongozi watakaowaongoza.
Anabainisha kuwa wasilisho lake linalenga kuelimishana, kukumbushana na kujadiliana ili polisi na waandishi wa habari wawe na lengo moja la kuimarisha amani, utulivu na usalama wakati wa uchaguzi. Waandishi wa habari na jeshi la polisi wote wana majukumu ya kutekeleza wakati wa uchaguzi lakini ni vema kila mmoja kwa wakati wake akajua mipaka yake katika kutekeleza majukumu yao.
Akifafanua hayo, Misime anasema usalama ni pamoja na kujitambua, kujilinda kwa kuchukua tahadhari za kiusalama na kulindwa dhidi ya uhalifu, vitisho na vurugu. Misime anasema waandishi wa habari wana jukumu na mchango mkubwa kipindi cha uchaguzi, hivyo kutekeleza wajibu kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu, weledi na kutokutanguliza maslahi binafsi mbele pamoja na kuzingatia haki za binadamu, kutachangia kuondoa hofu ya watu kushiriki katika mchakato mzima wa uchaguzi.
Aidha, anasema ni wajibu wa waandishi kuzingatia weledi, maadili na miiko ya uandishi wa habari, kutoa taarifa sahihi, zenye uwazi na usawa, kuwa mstari wa mbele kutunza na kuhamasisha amani, utulivu na usalama, wakati wa uchaguzi. Anasema ukiacha wajibu wa waandishi, polisi pia wana wajibu na jukumu kubwa la kulinda amani na utulivu katika kipindi cha uchaguzi kwa kulinda maisha na mali, kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu, kupeleleza na kuhifadhi ushahidi na kukamata.
Anasema pia jeshi la polisi lina wajibu wa kuzingatia mikataba mbalimbali ya kikanda na kimataifa, kama vile itifaki ya Umoja wa Afrika kuhusu Demokrasia, Uchaguzi na Utawala Bora,kusimamia sheria na kuhakikisha zinafuatwa na kuheshimiwa sambamba na kuhamasisha na kuheshimu Haki za Binadamu.
Katika hatua nyingine Misime anayataka makundi hayo kulinda tunu za taifa ambazo ni amani, umoja, uhuru, mshikano, demokrasia, kwa kuepuka kuwa na majibu ya kufikirika na badala yake wazingatie uhalisia, weledi na ukweli wa jambo lililotokea.
Anasisitiza uwepo wa amani, utulivu na usalama wakati wa uchaguzi ni kichocheo cha kufanyika kwa uchaguzi huo kwa mafanikio kusudiwa na kuicha nchi ikiwa salama, kwani usalama wa wananchi wote wakiwepo waandishi wa habari unategemea sana kila mmoja kutambua kuwa hakuna haki isiyo kuwa na wajibu.
Kuhusu mwongozo wa vyombo vya habari na waandishi wa Habari wa uandishi wa habari za uchaguzi, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Dk Egbert Mkoko anasema kupitia mwongozo huo waandishi wanawajibu wa kuchapisha habari za kweli, sahihi, zinazoweza kuthibitishwa, na zilizohaririwa kikamilifu. SOMA: TCRA yahimiza umakini, weledi habari za uchaguzi
Pia, anasema wanatakiwa kuepuka kubashiri, kueneza uvumi, kupendelea, na kuripoti madai yasiyothibitishwa ama yaliyotengenezwa makusudi kwa nia ovu kwa kutumia teknolojia ya kidijiti. Dk Mkoko anasema waandishi wanatakiwa kuepuka maudhui yenye lengo la kuleta chuki, ubaguzi, kashfa, matusi, kuchochea vurugu, au migawanyiko ya kikabila, kikanda, kidini yenye kuhatarisha amani na usalama wa nchi.
“Madhumuni ya mwongozo huu ni kuweka msingi wa kitaaluma na kimaadili kwa vyombo vya habari, waandishi wa habari na wahusika wote wa sekta ya habari katika kipindi cha uchaguzi,” anasema Dk Mkoko. Anaongeza kuwa mwongozo huo unalenga kuhakikisha kunakuwa na haki, usawa, uwazi na weledi katika kutoa taarifa kwa umma ili kukuza demokrasia nchini.
Dk Mkoko anasema ni muhimu kwa waandishi wa habari kuzingatia mwongozo wa habari katika kuripoti uchaguzi Mkuu 2025 kwani unasisitiza nafasi na wajibu wa vyombo vya habari, waandishi wa habari, wasimamizi wa sekta ya habari na wadau mbalimbali katika kuhakikisha upatikanaji wa taarifa sahihi.
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, Patrick Kipangula anasema ni muhimu kwa waandishi wa habari wote wanaoripoti habari za uchaguzi kuhakikisha wanasajiliwa katika mfumo na kupata vitambulisho vyao kama ilivyoelekezwa.
Kipangula anasema hadi sasa zaidi ya waandishi wa habari 3,400 wamesajiliwa na bodi hiyo kwa maana ya kukidhi vigezo na kupata ithibati, pia waandishi 400 wamewasilisha taarifa zao na zinaendelea kufanyiwa kazi ili kupata ithibati.
PATA HABARI YA WWE MILIKI KIWANJA CHA KIWANDA PAMOJA NA £56,565,656,000 ONLINE LIVE HAPA + UCHAGUZI UKIISHA UTAGAWA KWA WATANZANIA £56,565,656,000 /56,000,000 maana tumekukabidhi NYOTA Yetu YA KUPATA HELA
PAMOJA NA bonanza la “We JuDGE….”
https://youtube.com/shorts/_jB1m_sfFuM?si=wSugXDCDnASW1bK6
Everybody can earn 220$/h + daily 1K… You can earn from 6000-12000 a month or even more if you work as a part time Work…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good eaning opportunity..go to this site home tab for more detail thank you…….
.
Reading This Article:———————- http://Www.Cash43.Com
PATA HABARI YA WWE MILIKI KIWANJA CHA KIWANDA PAMOJA NA £56,565,656,000 ONLINE LIVE HAPA + UCHAGUZI UKIISHA UTAGAWA KWA WATANZANIA £56,565,656,000 /56,000,000 maana tumekukabidhi NYOTA Yetu YA KUPATA HELA
PAMOJA NA bonanza la “We JuDGE….”
https://youtube.com/shorts/_jB1m_sfFuM?si=wSugXDCDnASW1bK6
I just got paid $22k working off my laptop this month!** And if you think that’s cool, my divorced friend has twin toddlers and made over $22620 her first month. details on this website**Want the secret?** Copy this Website and choose HOME TECH OR MEDIA…..
Here is I started_______ https://Www.CashHive1.Com