KAMATI ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii imepongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga Sh bilioni 8 kuanza kutelekeza mradi wa Kupanga, Kupima na Kumilikisha (KKK) katika eneo lililopo pembezoni mwa uwanja wa mpira wa Afcon uliopo kata ya Olmort Jiji la Arusha .
Pongezi hizo zimetolewa leo jijini Arusha na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Najma Murtaza Giga wakati kamati hiyo ilipotembela na kujionea eneo la mradi wa KKK pamoja na kujionea ujenzi wa uwanja wa Afcon unaojengwa kwaajili ya mashindano ya mpira mwaka 2027.
Ameipongeza wizara ya ardhi kwa kuja na mradi huo wa viwanja na kuongeza kuwa tukio hilo ni la kihistoria kwani ndani ya miaka miwili ya ujenzi wa uwanja huo wa Afcon si mbali hivyo serikali iharakishe ujenzi huo huko makazi ya wananchi yakipimiwa na kuanishwa shughuli mbalimbalimbali za maendeleo.
Naye Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya MakaziDeo Ndejembi amesema fedha hizo zimetolewa na wizara hiyo kwaajili ya ulipaji wa ekari 207 za awali kati ya ekari zaidi ya 4,575.5 zilizopo katika mpango wote huo ambapo uwanja wa Afcon pekee unakeri 83 .
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtahengerwa amesema kupangwa kwa mji huo ulio karibu na uwanja wa mpira unaendelea kujengwa utawezesha jji la Arusha kupaa kuichumi na kiutalii kutokana na fursa mbalimbali zilizopo ndani ya mkoa huo na kuwaomba wadau mbalimbali kushirikiana na Jiji la Arusha katika kuhakikisha maendeleo yanakuwa ikiwemo uchumi wa mwananchi mmoja mmoja kutokana na aina ya biashara watakazofanya.