Kamati yashauri matumizi gesi asilia yaongezwe nchini

DAR ES SALAAM :KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imetembelea kituo mama cha kushindilia gesi asilia cha Mlimani-CNG jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza namna kituo hicho kinavyoendesha shughuli zake na kutoa huduma kwa wananchi, huku ikiishauri Serikali kuongeza juhudi katika kuimarisha matumizi ya gesi asilia nchini.
Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea kituo hicho kilichopo chini ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Subira Mgalu, amesema gesi asilia ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi kupitia upatikanaji wa nishati nafuu na rafiki kwa mazingira.
Mbali na hayo ameiomba Serikali kuhakikisha inaongeza matumizi ya gesi asilia kwenye magari na majumbani ili kupunguza utegemezi wa mafuta ya petroli na dizeli huku akiwataka wawekezaji kuwekeza zaidi katika miundombinu ya CNG ili wananchi wengi waweze kufikiwa na kunufaike na huduma hiyo.

Aidha, ameishauri Serikali kuangalia utaratibu wa kuhakikisha magari ya taasisi za umma yanatumia CNG kwa lengo la kupunguza gharama za mafuta na kuongeza ufanisi wa matumizi ya fedha za umma, na kuitaka TPDC kuongeza vituo vya kujaza gesi asilia nchini ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema wamepokea maelekezo ya Mwenyekiti wa Kamati na kuahidi kuyafanyia kazi huku akiongeza kuwa TPDC kupitia Wizara ya Nishati inaendelea kutoa huduma ya gesi ya CNG katika maeneo mbalimbali ya nchi ili kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.

Amesisitiza kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha upatikanaji wa gesi asilia unaimarika zaidi, hatua itakayosaidia kupunguza gharama za usafiri, kuongeza matumizi ya nishati safi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.




Barua hii nzuri deadcation yake
https://youtube.com/shorts/ha3p2PG2Lys?si=qug_e2ahNYe6rqZN