Kanali Sawala akumbusha ulipaji kodi kwa hiari

MTWARA: MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala amewasihi wafanyabiashara mkoani humo kuendelea kulipa kodi kwa hiyari ili miradi mingi zaidi ya maendeleo iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na Serikali mkoani humo.
Hayo yamejiri leo Septemba 29, 2025 wakati wa uzinduzi wa dawati maalumu la uwezeshaji biashara Mkoa wa Mtwara uliyofanyika katika Manispaa ya Mtwara Mikindani, linaloendeshwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Mtwara.
Aidha, ameitaja baadhi ya miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa mkoani humo ikiwemo ujenzi wa barabara ya uchumi kutoka Mnivata- Tandahimba Newala hadi Masasi kilometa 160 unaoendelea kwa kiwango cha lami itayoenda kufungua fursa za kibiashara pamoja na shughuli mbalimbali za kijamii.
Pia Miradi mikubwa ya maji ikiwemo wa makonde uliyopo wilayani Newala utaohudumia wilaya tatu kama vile Newala, Tandahimba na Halmashauri ya Mji Nanyamba na mirdi na mingine.
“Mnaweza mkaona ni muhimu kiasi gani kodi yetu inavyotuletea maendeleo katika nchi yetu, haya yote yanawezekana ni kwasababu ya fedha ambayo inatokana na kodi yenu,”amesemwa Sawala
Meneja wa TRA mkoani humo Maimuna Khatib amesema lengo la dawati hilo ni kuwasaidia wafanyabiashara na wajasiliamali wote kukua na kutatua changamoto zao mbalimbali zinazowakabili ili siku moja waweze kushirikiana na TRA katika kuimarisha uchumi wa taifa.
Majukumu ya dawati hilo ikiwemo kuwatambua, kuwalea na kuwazesha wafanyabiashara wote waliyopo kwenye sekta rasmi na wale wasiyo kwenye sekta rasmi.
Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) mkoani humo, Mwajuma Ankoni ameiomba TRA kuwa dhamira yao ya kuwawezesha wafanyabiashara hao ikawe mfano hai na bora kwa taasisi zingine kuona umuhimu kuwashirikisha wafanyabiashara na wajasiliamali katika kukuza biashara na kipato cha wananchi, mkoa na taifa kwa ujumla.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoani humo, Hamza Licheta “Sisi wafanyabiashara tunawaahidi tunapofanya biashara ni matumaini yetu kuleta tija kwa serikali tunaamini biashara tukiitengenezwa vizuri tutaenda kulipa kodi vizuri”