Kapinga ataja vigezo vya ziada upelekaji umeme vitongojini

DODOMA: Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unatekeleza miradi ya umeme katika vitongoji kwa kuzingatia vigezo vya ziada ikiwemo ukubwa wa vitongoji, jimbo na mahitaji ya kiuchumi na kijamii.

Lengo la kuweka vigezo hivyo ni kuhakikisha kuwa kila jimbo linakuwa na vitongoji vingi vilivyofikiwa na nishati ya umeme.

Kapinga ameyasema hayo leo Mei 29, 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la la Mbunge wa Simanjiro, Christopher Olesendeka aliyeuliza kwamba Serikali imejipangaje kutekeleza miradi ya vitongoji kulingana na jiografia ya Wilaya ya Simanjiro ambapo umbali kutoka kitongoji kimoja hadi kingine ni zaidi ya kilometa kumi.

“Mheshimiwa Naibu Spika, tunatekeleza miradi hii ya vitongoji kwa kuzingatia vigezo vya ziada, tumeangalia ukubwa wa jimbo husika, ukubwa wa vitongoji na mahitaji ya kiuchumi na kijamii katika jimbo husika. Niwahakikishie Wabunge mtaona utofauti katika miradi hii tunayoitekeleza hivi sasa,” Kapinga.

Akijibu swali la Mbunge wa Nyasa, Stella Manyanya aliyeuliza kuhusu kitongoji cha Songea Pori kilichopo katika kijiji cha Lunyele  na kitongoji cha Nindi kilichopo kijiji cha Konganywita kufikishiwa nishati ya umeme, Kapinga amesema vitongoji hivyo vimefanyiwa upembuzi yakinifu na kubainika vinahitaji njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kati kwa umbali wa kilometa tatu.

Amesema Serikali inatarajia kuvipelekea umeme vitongoji hivyo kupitia Mradi wa Kupeleka Umeme Vitongojini Awamu ya Pili B (HEP IIB) ambao utekelezaji wake utaanza mwaka wa fedha 2025/2026.

Aidha, amemuagiza kuchukua hatua za ziada kwa Mkandarasi huyo kuhakikisha anatekeleza mradi huo kwa haraka na kwa weledi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button