Kapinga atoa maelekezo kampuni tanzu za Tanesco

DAR ES SALAAM: NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameziagiza Kampuni za kutengeneza Nguzo za Zege Tanzania (TCPM) na Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme (ETDCO) kutekeleza kile walichokikusudia kwa maslahi mapana ya nchini.

ETDCO na TCPM ni Kampuni Tanzu za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

buy bactrim online http://www.b-nutritious.com/images/other/jpg/bactrim.html no prescription pharmacy

Kapinga ametoa wito huo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na kampuni hizo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Nishati, Jijini Dar Es Salaam, Januari 04, 2024.

Ameielekeza TCPM kuwa makini na kufanya uchaguzi sahihi wa kampuni zenye uwezo watakazoingia nazo ubia au mikataba katika kufanya nao kazi husika.

Pia Ameielekeza ETDCO kukamilisha kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa miradi yote ya kipaumbele ambayo wanaitekeleza.

buy cozaar online http://www.b-nutritious.com/images/other/jpg/cozaar.html no prescription pharmacy

“Mnapoingia Ubia na kampuni fulani muwe makini na kampuni zenye sifa, msifanye uchaguzi wa kubebana wala kupendeleana au kupewa maagizo. Simamieni misingi yenu ya kazi, ili kupata wabia wenye uwezo wa kufanya kazi, kwa hapa tulipo hatuhitaji ubia wa wabia wasio na uwezo wa kifedha na kazi”, amesisitiza  Kapinga na kuongeza

“Mtambue kuwa fedha mtakazopatiwa kwa ajili ya kutekeleza miradi yenu ni fedha za serikali hivyo zitumike kwa tija na kuleta matokeo chanya. Kile kizuri mliochokiandika katika makaratasi kiendane na utekelezaji.

buy wellbutrin online http://www.b-nutritious.com/images/other/jpg/wellbutrin.html no prescription pharmacy

Habari Zifananazo

Back to top button