Kaukau kutozwa ushuru

DODOMA; SERIKALI inakusudia kutoza ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha Shilingi 50 kwa kilo ya crisps (kaukau) zinazozalishwa nchini, na shilingi 100 kwa kilo ya crisps zinazoingizwa kutoka nje ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba, wakati anawasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka 2025/26 bungeni leo Juni 12, 2025.