Wataalamu wa usingizi wapewa sifa KCMC

HOSPITALI ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) imeungana na dunia kuadhimisha Siku ya Usingizi na Ganzi Tiba Duniani kwa kusherehekea mchango wa wataalamu hao katika kuhakikisha upasuaji unafanyika kwa usalama.
Akizungumza na wafanyakazi na viongozi wa hospitali jana, Oktoba 16, 2025, Mkurugenzi Mtendaji, Prof. Gileard Masenga, aliwashukuru wataalamu wa usingizi na ganzi tiba. Alisema kuwa kazi yao mara nyingi haionekani machoni pa jamii, lakini ndio msingi wa upasuaji salama. “Ninyi ni mashujaa wasioonekana. Kila upasuaji salama unaanza na mtaalamu wa usingizi,” alisema.
Dk. Herman Ayesiga, Mkurugenzi mwenye dhamana ya Upasuaji, pia aliwapongeza kwa nidhamu na ufanisi wao, akisisitiza umuhimu wa kuendelea kutoa huduma bora kwa moyo wa kujituma. Viongozi wa idara hiyo walishukuru uongozi wa KCMC kwa kuwapatia rasilimali na vifaa vya kisasa, na kuahidi kuendelea kutoa huduma bora na salama kwa wagonjwa.
Maadhimisho haya yamekuwa fursa ya kutambua mchango muhimu wa wataalamu wa usingizi na ganzi tiba katika kulinda maisha ya wagonjwa na kuhakikisha kila upasuaji unafanyika kwa viwango vya kitaaluma. SOMA: Wataalamu wa ganzi, usingizi kujifunza njia za kisasa MOI
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com