Kenya: Miili yafukuliwa Kilifi

KENYA : TAKRIBANI miili mitano imefukuliwa kutoka makaburi ya kina kifupi katika pwani ya kaskazini mwa Kenya. Maeneo hayo yanahusishwa na wahanga wa itikadi kali za kidini.
Kamishna wa Kilifi, Josephat Biwott, amesema miili hiyo ilipatikana kwenye makaburi manne huku mengine 27 yakichunguzwa. Uchunguzi unaendelea katika eneo la Malindi karibu na Shakahola ambako awali mamia walifariki kutokana na kufunga kupita kiasi.
Mwezi Julai, Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma alisema waliokufa huenda walilazimishwa kufunga. Hadi sasa watu 11 wanachunguzwa kwa kuhusika na vifo hivyo. SOMA: Idadi watu waliokufa maporomoko Uganda yafikia 28