Kenya wadhibiti mlipuko wa ugonjwa usiojulikana

KENYA : WIZARA ya Afya nchini Kenya imeanza uchunguzi wa mlipuko wa ugonjwa usiojulikana ambao umeathiri zaidi ya watu 200 katika vijiji vitatu vya jimbo la Kisii, nchini Kenya.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya anayehusika na masuala ya afya ya jamii, Mary Muthoni, amesema kuwa maafisa wa serikali kwa kushirikiana na serikali ya jimbo la Kisii wamefika katika maeneo yaliyoathirika ili kuanza uchunguzi. Matokeo ya uchunguzi huo yanatarajiwa kutangazwa leo, tarehe 4 Machi, 2025.

Muthoni amebainisha kuwa dalili kuu za ugonjwa huo ni pamoja na kuhara damu, kutapika, homa kali, na maumivu makali ya kichwa.

Taarifa kutoka kwa wananchi zinaeleza kuwa vijiji vya Nyamarondo, Nyarigiro, na Nyabigege, vilivyopo katika eneo la Mugirango Kusini, ndizo zilizoathirika zaidi na mlipuko huu wa ugonjwa.

Kwa upande mwingine, vituo vya afya vimeripoti kwamba vinakutana na changamoto kubwa ya kushindwa kudhibiti wingi wa wagonjwa wanaohitaji matibabu, tangu ugonjwa huu ulipogundulika kwa mara ya kwanza takriban wiki tatu zilizopita.

Kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa, baadhi yao wanashirikiana vitanda, huku wengine wakihamishiwa kwenye vituo vya afya vya karibu kwa matibabu zaidi.

SOMA: KENYA: Wanawake 200 wapoteza maisha 2024

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button