Kihongosi apiga marufuku ‘faini ya funguo’ Arusha

ARUSHA: MKUU wa Mkoa wa Arusha, Kenani Kihongosi amepiga marufuku ‘faini ya funguo’ utozwaji ya sh, 30,000 inayotozwa baada ya mmiliki wa eneo husika kushindwa kulipa kodi mbalimbali ikiwemo kodi ya leseni na kodi ya huduma, zinazotozwa na halmashauri ya Jiji la Arusha kutokana na wafanyabiashara hao kushindwa kulipa kodi hizo kwa wakati.

Kihongosi amepiga marufuku hiyo jana wakati akiongea na wamiliki, wafanyakazi na watumishi jiji hilo ili kubaini changamoto zao na kutafuta majibu sahihi ikiwemo utunzaji wa amani ikiwemo usafi wa maeneo wanayofanyia kazi.

Amesema watakaothibitika kuchukua sh, 30,000 za faini za funguo kwa watumishi wa idara ya biashara kumi na moja waliopo Jiji la Arusha watachukuliwa hatua za kisheria kwani huo ni ukandamizaji kwa wananchi hao ambao wanaendesha maisha kupitia saluni wanazofanya kazi.

“Hii faini ya funguo haikubaliki sasa ukifunga saluni na kudai hela hizo kwa mwezi ni shilingi ngapi tutachukua hatua na lakini naagiza Jiji la Arusha kutenga maeneo ya wafanyakazi wa saluni ili kuhakikisha kila mmoja anapata riziki badala ya kugombana,”

Amesema watu wa saluni ni kada nzuri yenye wateja wengi hivyo wanapoona kunahabari tofauti za wateja wao watoe taraifa serikali ili hatua ziweze kuchukuliwa na kusisitiza kulinda amani kwa kutoa viashiria ambavyo havijakaa sawa kwani amani ya nchi ni tunu pekee.

Amesisitiza waajiri wa saluni kutoa mikataba ya ajira huku alisema Jiji la Arusha linatoa Sh bilioni 5.5  ya mikopo ya 10%  inayotolewa serikali kwa vijana, wanawake na makundi maalum kwa ajili ya kupata mikopo hiyo ili wajikwamue kiuchumi ambapo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, John Kayombo alisisitiza elimi hiyo kuendelea kutolewa ili watu mbalimbali waweze kupata mikopo

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button