Kilo mil 2 dawa za kulevya zakamatwa

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema katika kipindi cha mwaka jana, imekamata dawa za kulevya zaidi ya kilogramu milioni mbili ukilinganisha na mwaka 2023.

Mwaka 2023 ilikamata dawa za kulevya kilogramu milioni 1.9, kiasi hicho kimeongezeka kutokana na operesheni na doria zilizofanyika mwishoni mwa mwaka jana na kukamata kilogramu 673.2 za metham phetamine na heroini.

Akizungumza na waandi shi wa habari Dar es Salaam jana, Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo alisema kiasi hicho ni kikubwa ku wahi kukamatwa nchini.

Advertisement

“Niseme tu endapo kiasi hiki kingefanikiwa kusam bazwa kingeleta athari kubwa na kurudisha nyuma ustawi wa taifa letu,” alisema Lyimo.

Alisema katika operesheni iliyofanyika katika Bahari ya Hindi wamekamata raia nane kutoka Pakistani wakiwa na dawa za kulevya kilogramu 448.3 zilizokuwa zimefichwa ndani ya jahazi lililosajiliwa Pakistani kwa namba B.F.D 16548, huku kilogramu 224.9 zikikamatwa kwenye fukwe za Bahari ya Hindi, Dar es Salaam.

“Katika msako wetu tuli wakamata raia hao na katika mahojiano walikiri kuwa wao ni wafanyabiashara wa dawa za kulevya ambazo wanasafirisha kutoka Bara la Asia kisha kuletwa Afrika, yanapofika kwetu yanaanza kusambazwa maeneo mbalimbali ambayo yapo mbali na Bahari ya Hindi kwa kutumia usafiri tofauti na tayari wamefikishwa ma hakamani leo (jana),” alifa fanua Lyimo.

Aliongeza: “Jahazi lililo kamatwa limefanya kazi ya kusambaza dawa za kulevya kwa miaka 28 na lina uwezo wa kubeba tani nane kwa wakati mmoja”.

 

Alitoa wito wangu kwa wafanyabiashara wote wa dawa za kulevya waliokim bilia nje ya nchi kujisalimisha kwani mamlaka itafuatilia kila sehemu.

Lyimo alisema bangi ni dawa ya kulevya iliyokamat wa kwa wingi zaidi mwaka huo ikifuatiwa na metham phetamine, heroini na dawa tiba yenye asili ya kulevya aina ya Fentanyl, lakini pia kwa mara ya kwanza dawa mpya ya kulevya aina ya 3-4 Methylene-Dioxy-Pyrova lerone (MDVP) ilikamatwa nchini.

Aidha, alisema ni vyema jamii ikaepuka matumizi ya mirungi kwani husababisha saratani ya utumbo, ya koo na meno kung’ooka.

Katika hatua nyingine, Lyimo alisema serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, wameongeza vituo viwili vya matibabu katika mikoa ya Pwani na Tanga, na hivyo kufanikisha kuwa na jumla ya vituo 18 vya MAT nchini na tayari vimesajiliwa na vinawahudu mia waraibu 18,170.

Alisema zimeongezeka nyumba sita za upataji nafuu na hivyo kufikia nyumba 62 ambazo waraibu 17,230 walipata huduma za utenga mao na zaidi ya 600,000 wa lihudumiwa katika vitengo vya afya ya akili vilivyopo kwenye hospitali za wilaya, mikoa na hospitali za rufaa za kanda.

Kuhusu vipaumbele vya 2025, Lyimo alisema DCEA itajikita zaidi kuimarisha zaidi udhibiti wa dawa za kulevya kwa kuongeza ushirikiano wa kimataifa na matumizi ya teknolojia za kisasa kufuatilia mitandao ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya, utoaji wa elimu kwa umma ili kuhamasisha wananchi kushiriki kutoa taarifa za watu wanaojihusi sha na dawa za kulevya na kujiepusha na biashara na matumizi yake.