Kinana amsifu kwa bidii Samia

DAR-ES-SALAAM : MAKAMU Mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amesema mgombea urais wa chama hicho, Samia Suluhu Hassan anajituma.

Kinana alisema hayo kwenye mkutano wa kampeni jijini Arusha jana. Alisema mgombea huyo amefanya kazi kubwa katika kipindi cha miaka minne. Kinana alisema alipoingia madarakani Machi mwaka 2021, Samia alikuta mafungu matatu ya ahadi zinazosubiri kutekelezwa zikiwemo za CCM yenyewe na mgombea wake awamu iliyopita.

“Inahitaji kiongozi mwenye utulivu, aliyejipanga vizuri kuhakikisha kazi zote hizo zinakamilishwa kwa wakati. Pamoja na kuingia madarakani kwa mshtuko na kukuta ahadi nyingi, Rais Samia amefanya kazi ya kutukuka,” alisema. Kinana alibainisha siri kubwa iliyomfanya Samia atekeleze ahadi nyingi kiasi hicho, kuwa ni kujituma kwake na kujitolea kwa moyo mkunjufu kufanya kazi hizo kwa maslahi ya Watanzania. Alisema matokeo ya kazi hizo kila Mtanzania ni shahidi, kwa sababu ndio wanaonufaika kwa kiasi kikubwa na kazi hizo.

“Ahadi zote alizozitoa hatimaye amezikamilisha kwa asilimia 100. Katika kipindi hiki cha kampeni, Rais Samia anaeleza mambo matatu, la kwanza ni kueleza mafanikio na kazi kubwa iliyofanywa na serikali yake. Pili, ni kuleta matumaini kwa Watanzania kutokana na kile kinachoenda kutekelezwa katika miaka mitano ijayo,” alieleza Rais Samia.

Alitoa siri kuwa hata kaulimbiu ya uchaguzi wa mwaka huu ya ‘Kazi na Utu Tunasonga Mbele’ inamuelezea Rais Samia kwa undani kutokana na utu alionao, ambao msingi wake ni haki. Ndio maana aliunda Tume ya Jaji iOthman Chande kuchunguza mifumo ya utoaji wa haki nchini. SOMA: Mfumo wa stakabadhi ghalani utasimamiwa

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button