Kiruswa aishukuru serikali ya CCM kuthamini wafugaji

ARUSHA : MGOMBEA ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Longido, Dk Steven Kiruswa ameishukuru serikali kwa kuithamini sekta ya mifugo na wafugaji. Dk Kiruswa alisema hayo katika Uwanja cha Sheikh Amri Abeid Arusha kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Samia Suluhu Hassan.

Amesema Rais Samia akiwa madarakani, ndiye kiongozi aliyetambua umuhimu ya wananchi wa jimbo hilo ambao asilimia kubwa ni wafugaji, kwa kumtuma Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa kutangaza kwamba maeneo yao ya malisho yatabaki kuwa salama.

“Wafugaji ambao ndio asilimia kubwa ya jamii ya jimbo hili wanakuomba watakapokuchagua tena, wanaomba maeneo yao yapimwe, yasajiliwe na wasaidiwe miradi ya maji kwa ajili ya mifugo yao kama mabwawa na visima virefu na kuendelea kuwatengea maeneo ya ufugaji,” alisema Dk Kiruswa.

Alisema serikali ya Rais Samia imefanya maboresho mengi kwenye sekta ya nishati, ambayo umeme umefika kila kijiji na hata katika maeneo yenye migodi. Dk Kiruswa alisema katika miaka minne ya uongozi wake, alitoa Sh bilioni 26 kwa ajili ya kujenga mradi wa maji kutoka Mlima Kilimanjaro kwenye Mto Simba kwenda Longido hadi Namanga na tayari aliuongezea thamani mradi huo kwa kutoa Sh bilioni 14 zilizoelekezwa kwenye chanzo cha maji Bonde la Sinya. SOMA: Kinana amsifu kwa bidii Samia

“Longido ambayo ilikuwa ni moja ya wilaya zenye ukame nchini, ulipoingia madarakani upatikanaji wa maji katika maeneo ya vijiji na miji ulikuwa ni asilimia chini ya asilimia 56 lakini sasa umefikia zaidi ya asilimia 70,” alisema. Pia, alisema wananchi wa Longido wameamua na wamedhamirimia kumchagua kwa asilimia 100, kwa sababu jimbo hilo lilishaweka historia ya kukipigia kura chama hicho kwa asilimia zote.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button