SMZ yapongezwa uwekezaji sekta ya afya

KIZIMKAZI, ZANZIBAR: WAKAZI wa Kizimkazi Mkunguni wameeleza furaha na fahari yao kufuatia upatikanaji wa huduma bora za afya kupitia Kituo cha Afya kilichojengwa kwa viwango vya kisasa na chenye hadhi ya hospitali, kinachotoa huduma zote bure kwa wananchi.

Kituo hicho kilizinduliwa rasmi Januari 3, 2025 na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk Jakaya Mrisho Kikwete, na kilianza kutoa huduma Februari 1, 2025. Tangu kuanza kwa huduma zake, idadi ya wagonjwa imeongezeka kutoka wastani wa watu 70 kwa siku hadi kufikia zaidi ya watu 3,000 kwa sasa.

Akizungumza na HabariLEO wakati wa ziara ya wahariri waliotembelea miradi ya maendeleo Zanzibar, Daktari Mkuu wa kituo hicho, Dk Tamimu Hammad Said, alisema huduma zote zinatolewa bila malipo yoyote.

“Wagonjwa wanaolazwa wanapata huduma zote bure, ikiwemo chakula. Kina mama wanaojifungua pia wanahudumiwa bila gharama yoyote. Tunajivunia kutoa huduma bora kwa wakazi wote wa eneo hili na maeneo jirani,” alisema Dk Tamimu. SOMA: Mariam Mwinyi azindua Zanzibar Afya Week

Aliongeza kuwa kituo hicho kimekuwa msaada mkubwa kwa jamii kwa kupunguza vifo vya wajawazito na watoto, sambamba na kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya za msingi kwa wananchi.

Wakazi wa Kizimkazi nao walitoa pongezi kwa Serikali kwa uwekezaji huo, wakisema kuwa huduma bora na za karibu zimewasaidia kupunguza gharama na usumbufu wa kusafiri umbali mrefu kufuata matibabu.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button