Kombo atangaza fursa ajira 50,000 nje ya nchi

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amesema Tanzania imepokea mkataba wa ajira 50,000 za nje za nchi.
Balozi Kombo amesema hayo kwenye mkutano wa kampeni za mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan katika Viwanja vya Tanesco Buza wilayani Temeke jana. “Tumepokea taarifa ya mkataba wa ajira kwa ajili ya vijana wa Kitanzania wenye umri wa miaka 20 hadi 35 kufanya kazi nchi za nje na kuna ajira nyingine 20,000 zipo njiani kuja. Hivyo, vijana mjitayarishe, Samia anafanya kwa vitendo na si kwa maneno,” alisema. Balozi
Kombo amesema Serikali ya Awamu ya Sita katika ilani iliyopita iliahidi ajira 5,000,000 na ikatekeleza zaidi ya kiwango hicho. Ameongezea kuwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM 2025-2030 malengo ya fursa za ajira yameongezwa hadi kufikia 8,000,000. SOMA: Mwinyi aahidi ajira kwa vijana




Working from home with kids used to sound impossible, but now I earn between $90 and $500 per hour! My friend was making $22K monthly and helped me start — check it out here
https://dailycash21.blogspot.com/