Koola: Tutashirikiana kuipaisha Vunjo

KILIMANJARO: MGOMBEA Mgombea Ubunge wa Jimbo la Vunjo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Enoch Koola, amesema amefurahishwa na mapokezi makubwa aliyoyapata kutoka kwa wananchi wa jimbo hilo, akiahidi kushirikiana nao katika kuleta maendeleo.
Kupitia ujumbe wake alioutoa leo Koola amesema: “Wanavunjo wenzangu, moyo wangu umejaa furaha kwa mapokezi mliyonipa. Nimeona shauku yenu, nimesikia sauti zenu na nimeguswa na matumaini yenu. Tushirikiane kuiinua Vunjo ili kesho iwe bora kuliko leo.”
Amesisitiza kuwa dhamira yake kubwa ni kushirikiana na wananchi katika kujenga Vunjo yenye maendeleo.
Koola pia alionesha matumaini makubwa kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba, akiwataka wananchi wa Vunjo kujitokeza kwa wingi na kumchagua ili kupeleka sauti yao bungeni.
This really answered my problem, thank you!