‘Kufikisha ujumbe kwa maandamano hakuleti chakula’

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema kunung’unika na kufikisha ujumbe wa changamoto mbalimbali kwa njia ya maandamano kumepitwa na wakati.

Amesema Watanzania wanataka maendeleo ukiwemo ujenzi wa miundombinu muhimu ambayo itarahisisha shughuli za kiuchumi na ajira kwa wananchi.

Wasira amesema hayo leo Septemba 28, 2025 alipokuwa akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM kutoka majimbo ya Vunjo na Moshi Vijijini, mjini Moshi.

“Wewe unanung’unika tu maandamano utakula maandamano, tunataka reli ya kisasa kwa sababu katika dunia inayoendelea tofauti ya nchi zetu na nchi zilizoendelea ni miundombinu, ukifika tu unaiona barabara pana, kuna reli inakwenda ‘speed’ kwa hiyo barabara inakwenda speed.

“Hakuna biashara ya kisasa ya kutunza vitu kwa matenga umebeba kichwani, hiyo ni biashara ya zamani, biashara ya kisasa ni ile inayokwenda ‘very fast’ and speed.”

Kwa mujibu wa Wasira,  Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025-2030 inaelekeza reli kuunganisha Pugu (Dar es Salaam), Tanga na Arusha kupitia Mkoa wa Kilimanjaro.

“Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inataka reli iunganishe Pugu, Tanga na Arusha kupitia Kilimanjaro, na sisi Musoma kule hata isipokuja miaka mitano hii inayokuja mpaka Arusha tunaisubiri na ili tuipate tutahakikisha CCM inaendelea kushinda.

“Ilni inasema sasa Musoma tujenge bandari kama hatua ya kwanza ya kupokea reli na reli ikifika itakuwa inatokea Arusha inatuunganisha na Tanga na sisi tutafanya biashara kati ya Musoma na Port bell ya Uganda,” amesema.

Amebainisha kuwa, kwa namna hiyo vijana watapata kazi kwenye reli na kwamba ni muhimu kutafuta majibu ya matatizo mapya mara kwa mara.

Amesisitiza kuwa, zipo njia sahihi na bora zaidi kufikisha ujumbe mahali husika hususan kwa njia ya amani.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button