Kumekucha maonesho ya vitabu Dar

DAR ES SALAAM :JAMII imehimizwa kusoma vitabu ili kutunza fikra,kuhifadhi maarifa ya kitaifa pamoja na kutambua hadhi ya waandishi wa kitanzania ili kuwe na kizazi bora kinachotambua thamani ya yaliyohifadhiwa vitabuni.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam  na Dk  Mboni Ruzegea, Mkurugenzi Mkuu wa Maktaba ya Taifa (TLSB) na kueleza kuanzia Novemba 21 hadi 26 kutakuwa na maonesho ya Kitaifa ya 32 ya Vitabu Tanzania yatakayofanyika Maktaba Kuu ya Taifa.

” Maonesho haya yana malengo kadhaa muhimu kwanza ni kuonesha umma na ulimwengu, utajiri wa maaandishi lakini pia utajiri wa utamaduni, utajiri wa sanaa na historia na maarifa tuliyonayo kama Taifa.

“Lakini lengo lingine ni kunadi sasa huo utajiri tulinao lakini unafahamika, kwa hiyo lengo letu ni kunadi hii historia na tunu ya taifa, kupitia maandishi na kazi bunifu  za waandishi wetu wa hapa nchini, kuhamasisha jamii kupenda kusoma vitabu kama nguzo ya maarifa  weledi na fikra pevu,” amesema.

Amesema pia lengo lingine ni kukutanisha wadau wa elimu, wadau wa utamaduni, wachapishaji  ili kujenga mikakati endelevu ya usomaji pia uandishi na uhifadhi wa maarifa  hapa nchini, kwani kuna machapisho mengi hayajulikani.

Naye Hermes Damian Mwenyekiti wa Chama cha Wachapishaji Vitabu Tanzania (PATA), amesema maonesho hayo ni fursa kueleza ulimwengu kipi  kimefanyika na kuwapa uelewa zaidi kupitia vitabu.

Amesema miongoni mwa nchi zitakazoshiriki maonesho hayo ni Kenya,Malawi na nchi nyingine kama  Ufaransa,Canada, Swedeni na Irani.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Nowadays earning money online is very easy . Eanrs every month online more than $17k by doing very easy home based job in part time u can also do this simple online Job by visiting websiteMore Details For Us→→  http://www.job40.media

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button