Lagos kuandaa maonesho ya IATF 2027

ALGIERS, Algeria: Jiji la Lagos litaandaa maonesho makubwa ya tano ya Kibiashara Afrika (IATF) yatakayofanyika mwaka 2027, waandaaji wa maonesho hayo wametangaza katika siku ya kwanza ya maonesho hayo yanayofanyika Algiers nchini Algeria.
Rais wa zamani wa Nigeria na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la IATF, Olusegun Obasanjo amepongeza Lagos na kauitaka kujiandaa kupokea wageni nchini Nigeria.
Rais wa Angola na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, João Lourenço, ametuma salamu za pongezi kwa waandaaji wa maonesho hayo na kusema yamekuwa chachu ya maendelea kwa Afrika.



