Ligi ya vijana yashika kasi Arumeru

LIGI ya soka kwa vijana walio na umri chini ya miaka 13 itaeendelea kuchezwa Jumamosi  Septemba 6 katika viwanja vya shule ya kimataifa ya Kennedy House vilivyopo Usa River wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Katika michezo itakayochezwa wikiendi hii kwa umri wa miaka 13 timu ya Arusha Young stars itacheza dhidi ya Satino Academy, Mirrior Academy dhidi ya Follow your dream, Chuga boys Academy dhidi ya Arusha youth Academy huku Young boys Academy watacheza na Peace Youth Academy ambapo mechi zote zitachezwa katika viwanja wa Kennedy house.

Timu nane za vijana walio na umri chini ya miaka 13 zinashikiri mashindano ya soka yanayafanyika yakiwa na lengo la kutambua na kuibua vipaji vya watoto wanaochipukia.

Mashindano hayo ya vijana kwa ya ‘Arumeru youth league U13 2025’ yameandaliwa na kituo cha ya michezo cha Young boys Academy Tanzania yakilenga kuibua na kuendeleza vipaji vya watoto kuanzia ngazi ya chini yanaenda sambamba na ya vijana walio chini ya miaka 13 ambayo yanafanyika kwa pamoja kila wikiendi katika viwanja tofauti.

Ligi hiyo inahusisha vijana chini ya umri wa miaka 13 inazikutanisha timu za Satino Academy,Chuga boys Academy,Arusha New star Academy,MirriorAcademy,Peace Academy,Follow your dream academy ,Arusha Youth na Young boys Academy.

Viwanja vitatu vinatumika katika Ligi hiyo ya U13 ambavyo ni Aim Mall, Kennedy house na Young boys Academy na kila wiki timu zitacheza katika kiwanja kimoja.

Wakati huo huo ligi ya vijana chini ya miaka 11 nayo itaendelea jumamosi hii kwa CTIDO kucheza dhidi ya Black eagle Academy huku Young boys Academy itakuwa mwenyeji wa Satino Academy na mchezo wa tatu utazikutanisha Usa youth Academy dhidi ya Peace Academy mechi zote uwanja wa Baraa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button